Harambee Stars wawekwa kundi moja na Cameroon, kundi J kwa mechi za kufuzu Afcon 2025

Timu mbili kutoka kwa kila kundi zitafuzu kwa kombe la Bara Afrika 2025 nchini Morocco

Muhtasari

•Harambee Stars wameekwa kwenye kundi J pamoja na Zimbabwe,Namibia  na Cameroon  kwenye mechi za kufuzu kombe la bara Afrika[Afcon 2025] kule Morocco.

•Mechi hizo zinaratibiwa kuanza Septemba mosi hadi  Novemba mwaka huu.

Image: HISANI

Timu ya taifa ya kandanda ya Kenya Harambee Stars imewatambua wapinzani wao kwa mechi zijazo za kufuzu AFCON 2025

Droo hio ilifanyika nchini Afrika Kusini  Julai 4 ,2024 kwa usaidizi wa  kocha  wa Ivory  Coast,Emerse Fae na gwiji wa soka wa Morocco ,Marouane Chamakh .Mechi hizo  zitafanyika kuanzia Septemba mosi hadi Novemba mwaka huu.

Kenya itakuwa mbioni  kujaribu kufuzu kwa michuano hio kwa  mara ya saba, baada ya kukosa kufuzu kwa makala ya 2023 kutokana na marufuku ya mwaka mzima waliyowekewa na FIFA mwaka wa 2022.

Kenya wamepangwa Kundi J, ambapo watakuwa wakicheza dhidi ya Zimbabwe, Namibia na Cameroon lengo lao likiwa ni kufuzu kwa mara ya kwanza tangu 2019.

Sadfa iliyoje,kwani Kenya iliwekwa pamoja na Cameroon katika mechi za kufuzu 2023 lakini haikukabiliana nayo kutokana na kupigwa marufuku, na hivyo itakuwa na nafasi ya kukabiliana nao tena.

Kenya imekabiliana na Zimbabwe mara mbili mwaka huu, na kuibuka washindi mara zote mbili. Pia watakuwa na matumaini ya kurekebisha makosa ya mechi ya kufuzu AFCON 2013 dhidi ya Namibia, ambapo hawakuweza kuwafunga nyumbani na ugenini.

Afcon 2025 itakuwa inaanza Disemba 21 na kukamilika Januari 18, 2025.

Hii hapa ni orodha kamili:

 Kundi A:Tunisia,Madagascar, Comoros,Gambia

Kundi B:Morocco, Gabon ,Central Africa Republic, Lesotho

Kundi C :Egypt ,Cape Verde, Mauritania ,Botswana

Kundi D:Nigeria ,Benin, Libya ,Rwanda

Kundi E :Algeria, Equatorial ,Guinea,Togo,Liberia

Kundi F: Ghana ,Angola,Sudan ,Nigeria

kundi G: Ivory Coast, Zambia ,Sierra Leone, Chad

Kundi H :DR Congo, Guinea,Tanzania, Ethiopia

Kundi I: Mali ,Mozambique ,Ginea Bissau, Eswatini

Kundi J :Cmeroon, Namibia ,Kenya ,Zimbabwe

Kundi K :South Africa ,Uganda, Congo ,South Sudan

Kundi L:Senegal, Burkina Faso, Malawi ,Burundi