Robo fainali za Euro: Ujerumani dhiidi ya Uhispania,Ureno dhidi ya Ufaransa 2024

Mechi za kwanza za hatua ya robo fainali katika mashindano ya Euro 2024 zitachezwa leo.

Muhtasari

•Ujerumani itatifuana na Uhispania kuanzia saa moja usiku huku Kylian Mbappe akiratibiwa kuwaongoza Ufaransa watakapochuana na Ureno yake Christiano Ronaldo,saa nne usiku.

•Kocha wa Uhispania De la Fuente ametania kuwa watajaribu kumfunga Toni Kroos miguu ili kumzuia kupiga pasi nyingi.

Uhispania washerehekea bao dhidi ya Italia
Image: HISANI

Mechi za hatua ya robo fainali katika mashindano ya Euro 2024 zitachezwa leo huku Uhispania wakimenyana na Ujerumani,Ureno dhidi ya Ufaransa.

Ujerumani na Uhispania zitachuana mjini Stuttgart  kuanzia saa moja jioni saa za afrika mashariki.Mechi hiyo, marudio ya fainali ya Euro 2008 ,Uhispania  ilishinda 1-0  mjini Vienna, kwa hivyo inaahidi kuwa ya kusisimua.

Uhispania, wakiwa na wachezaji wawili wa kusisimua Lamine Yamal na Nico Williams kwenye 'wings', wametinga robo fainali kwa kushinda mara nne katika michezo mingi, mabao tisa ya kufunga na moja pekee ya kufungwa.

Kwa upande mwingine, Ujerumani pia wametinga hatua ya nane bora, huku Jamal Musiala akiwa bora katika safu ya ushambuliaji naye Toni Kroos akivuta safu ya kati akijiandaa kustaafu baada ya shindano hilo.

Kocha mkuu wa Ujerumani ,Julian Nagelsmann,kwenye mahojiano na waandishi wa habari aliwalinganishwa Yamal na Jamal Musiala huku akisema;

"Makini yangu ni kidogo kwa Yamal, zaidi kwa Jamal,tunaweza kufanya kitu katika kushambulia wenyewe. Tunataka kushambulia na kufanya maisha kuwa magumu kwao."

Pia walikutana katika hatua ya makundi kwenye Kombe la Dunia la 2022, wakitoka sare ya 1-1 ambayo ilichangia Ujerumani kuondolewa katika raundi ya kwanza.

 Uhispania labda wana mchezaji bora zaidi duniani wa kiungo Rodri, lakini kocha wao, Luis de la Fuente, alikiri kuwa wanahofia kipaji cha Kroos.

"Tulifikiria kumfunga Kroos miguu pamoja, lakini sina uhakika kama UEFA itaniruhusu," alitania. "Tunajua jinsi Kroos anavyofanya. Tutajaribu na kuhakikisha kuwa hana nafasi ya kupokea mpira na tutapunguza chaguzi zake za kupiga pasi."

Washindi wa mechi hiyo watatinga nusu fainali dhidi ya Ufaransa au Ureno, ambao watamenyana mjini Hamburg saa nne usiku. Ni pambano lingine la uzito wa juu kati ya pande mbili zinazopendwa sana, pamoja na marudio ya fainali ya Euro 2016, wakati Ureno ilipoichapa Ufaransa 1-0 katika muda wa ziada mjini Paris.

Ufaransa wametinga robo fainali ya sita katika michuano saba mikubwa iliyopita licha ya kwamba hakuna mchezaji wao aliyefunga katika mchezo wa wazi.

Kocha wa Ureno Roberto Martinez, alisisitiza kuwa lengo haliwezi kuwa kwa mastaa hao wawili [Christiano Ronaldo na Kylian Mbappe]

"Soka ni mchezo wa timu, hii si mechi ya watu wawili, ni wachezaji wawili wa ajabu ambao wana ushawishi mkubwa kwenye mchezo duniani kote, na ushawishi huo utaendelea, lakini kesho tutahitaji kiwango cha juu kabisa cha timu. tunapaswa kushinda," Martinez alisema.