logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Klabu ya Arsenal yawaaga wachezaji wake wawili

Kwa upande wa beki Nuno Tavares, aliachiliwa kujiunga na klabu ya Italia Lazio Roma kwa mkopo wa msimu mzima.

image
na Samuel Maina

Michezo16 July 2024 - 10:13

Muhtasari


  • •Lokonga amejiiunga na Sevilla ya Uhispania kwa mkopo wa msimu mzima huku klabu hiyo ya Laliga ikiwa chaguo la kumnunua kwa euro milioni 12.
  • •Kwa upande wa beki Nuno Tavares, aliachiliwa kujiunga na klabu ya Italia Lazio Roma kwa mkopo wa msimu mzima.

Klabu ya soka ya Arsenal imetangaza kuondoka kwa wachezaji wawili, kiungo wa kati Albert Sambi Lokonga na beki wa kushoto Nuno Tavares.

Klabu hiyo yenye maskani yake London ilithibitisha Jumatatu kwamba wachezaji hao wawili waliojiunga nao mwaka wa 2021 wameondoka klabu hiyo kwa mkopo.

Lokonga amejiiunga na klabu ya Sevilla ya Uhispania kwa mkopo wa msimu mzima huku klabu hiyo ya Laliga ikiwa chaguo la kumnunua kwa euro milioni 12.

"Hatua hii inayofuata katika taaluma ya Sambi inawakilisha fursa nzuri kwa kiungo wetu wa kimataifa wa Ubelgiji kutimiza uwezo wake zaidi kwa kushindana kwa kiwango cha juu katika ligi kuu ya Uropa. Kila mtu katika Arsenal anamtakia kila la kheri Sambi msimu huu ujao akiwa na Sevilla. Mkataba wa mkopo unategemea kukamilika kwa michakato ya udhibiti," Arsenal FC ilisema katika taarifa.

Inaripotiwa kuwa mshahara kamili wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 24 utalipwa na Sevilla FC.

Kwa upande wa beki Nuno Tavares, aliachiliwa kujiunga na klabu ya Italia Lazio Roma kwa mkopo wa msimu mzima.

Arsenal ilisema kuwa dili hilo la beki mwenye umri wa miaka 24 linategemea kukamilika kwa taratibu za udhibiti.

"Hatua hii katika maisha ya Nuno ni fursa nzuri ya kujiendeleza zaidi kwa kupata uzoefu muhimu katika Serie A na kandanda ya Italia. Kila mtu Arsenal anamtakia Nuno kila la heri msimu huu ujao akiwa na Lazio. Mkataba wa mkopo unategemea kukamilika kwa michakato ya udhibiti," Arsenal ilisema.

Inaripotiwa kuwa Lazio imetakiwa kumnunua mchezaji huyo wa Ureno baada ya kumalizika kwa muda wa mkopo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved