Mbappe atambulishwa kama mchezaji mpya wa Real Madrid mbele ya mashabiki zaidi ya 80k

Los Blancos walitangaza hivi majuzi kwamba atavaa jezi namba tisa katika msimu wake wa kwanza katika klabu hiyo, ambayo iliachwa na Karim Benzema baada ya msimu wa 2022-23.

Muhtasari

• Matangazo ya Real Madrid yalionyesha Mbappe aking'aa kwenye vyumba vya kubadilishia nguo akiwa amevaa shati lake jeupe na kuwaandalia umati wa mashabiki waliosimama.

• Rais wa klabu Florentina Perez pamoja na magwiji Zinedine Zidane na Pirri walimuongoza Mbappe na kuwasalimia wafuasi wake.

KYLIAN MBAPPE
KYLIAN MBAPPE
Image: X

Baada ya ngoja ngoja ya muda mrefu, hatimaye Mfaransa Kylian Mbappe ametambulishwa mbele ya mashabiki 80,000 wa Real Madrid kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu kama mchezaji mpya.

Matangazo ya Real Madrid yalionyesha Mbappe aking'aa kwenye vyumba vya kubadilishia nguo akiwa amevaa shati lake jeupe na kuwaandalia umati wa mashabiki waliosimama.

Rais wa klabu Florentina Perez pamoja na magwiji Zinedine Zidane na Pirri walimuongoza Mbappe na kuwasalimia wafuasi wake.

Nyota huyo wa Ufaransa alikamilisha uhamisho wake kutoka PSG mapema msimu huu wa joto baada ya misimu saba katika mji mkuu wa Ufaransa ikiwa ni moja ya sakata za uhamisho wa muda mrefu zaidi katika kandanda zikifikia kilele.

Amekubali kukatwa mshahara mkubwa baada ya kusaini mkataba wa miaka mitano, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 akipokea kitita cha pauni milioni 12.8 kwa msimu akiwa Madrid, chini ya pauni milioni 21.4 alizopata Paris.

Los Blancos walitangaza hivi majuzi kwamba atavaa jezi namba tisa katika msimu wake wa kwanza katika klabu hiyo, ambayo iliachwa na Karim Benzema baada ya msimu wa 2022-23.

Mbappe alivaa nambari 7 kwa muda mwingi wa maisha yake ya Paris Saint-Germain lakini jezi hiyo kwa sasa ni ya Vinicius Junior akiwa Madrid.

Wakati huo huo, Mbappe alikuwa mchezaji nambari 10 wa Ufaransa kwenye Euro 2024 - nambari ambayo imekuwa ya Luka Modric huko Bernabeu tangu 2017.

Ufaransa ilitolewa kwenye Euro 2024 katika hatua ya nusu fainali na Uhispania.

Madrid walikuwa wakisubiri hadi ushiriki wa Mbappe wa Euro umalizike kabla ya kutangaza mipango yao ya kumtambulisha rasmi.

Fowadi huyo kwa muda mrefu amekuwa akihusishwa na kuhamia Real Madrid na nusura ajiunge na Los Blancos msimu wa joto wa 2022, kabla ya kurejea kwa dakika za lala salama na kusaini mkataba mpya na klabu hiyo ya Ligue 1.