Klabu ya Chelsea ilitoka sare ya 2-2 kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Wrexham huku Christopher Nkunku na Lesley Ugochukwu wakicheka na wavu.
Kwenye mazungumzo na wanahabari,meneja wa Chelsea Enzo Maresca alisema timu yake huenda ikafungwa mabao msimu huu ikiwa itacheza kuanzia nyuma baada ya makosa mawili ya safu ya ulinzi katika sare ya 2-2 na Wrexham.
Maresca aliulizwa kuhusu kuruhusu kufungwa mabao kupitia mtindo wake wa uchezeshaji, ambao ni kumiliki mpira kutoka nyuma kwenda mbele.
"Tunatumai, sio nyingi sana. Ni moja ya njia hatari za uchezeshaji..." Maresca alisema.
Kocha huyo wa zamani wa Leicester mwenye umri wa miaka 44 alisema hana mpango wa kubadilisha mfumo wake wa uchezaji.
"Sina shaka. Nadhani utakubali kwa njia tofauti, kwa hivyo unahitaji kuamua ni njia gani unahitaji. kuruhusu goli.Wakati mwingine timu ambazo zinajaribu kujenga kutoka nyuma huruhusu mabao lakini nadhani utafunga zaidi ya unavyoruhusu.'
Aliongeza; "Kwa hakika, tulifanya mambo mengi ambayo tunaweza kuboresha, lakini tulianza wiki mbili zilizopita. Usiku wa leo ilikuwa muhimu kuanza kuona utambulisho wa timu."
Hata hivyo ,Maresca alidai kuwa lazima avumbue ujuzi zaidi hasa muda unaposonga ;
"Katika wakati huu, tulianza wiki mbili zilizopita, ni muhimu sisi kama wafanyikazi na watu kuanza kuona utambulisho wa timu. Usiku wa leo ilikuwa wazi kabisa. Kwa hakika tutaongeza suluhisho zaidi."
Mechi ijayo ya kirafiki ya Chelsea itakuwa dhidi ya Celtic Julai 27 ,2024,kabla ya kukutana na Club America Agosti 1 kisha Manchester City Agosti 4.
Klabu hio pia itachuana na Real Madrid Agosti 7 kabla ya kufunga mechi za kirafiki dhidi ya Inter Milan,Agosti 11.