Mfahamu Filip Jorgensen,Golikipa anayehusishwa kuhamia Chelsea

Kocha Maresca anatafuta kipa ambaye anafanya vyema akiwa na mpira miguuni mwake.

Muhtasari

•Chelsea ipo kwenye harakati za kumsajili kipa wa Villareal,Filip Jorgensen  kwa thamani ya €20m pamoja na nyongeza.

•Kutokana na mtindo wa uchezaji ambao Enzo Maresca anapanga kutumia msimu ujao,huenda Filip Jorgensen akawa jawabu kamili.

Filip Jorgensen ( Kipa wa Villarreal)
Image: Facebook

Klabu ya Chelsea ipo mbioni kumsajili kipa wa Villareal Filip Jorgensen ambaye amekuwa nguzo muhimu kwa klabu hio ya Uhispania.

Mkataba uko katika hatua za mwisho na Villareal,hii ni baada ya Chelsea kuboresha pendekezo lao lenye thamani ya €20m pamoja na nyongeza.

Mwanahabari nguli wa spoti,Fabrizio Romano alisema;

"Chelsea na Villareal wanajadili muundo wa mkataba ,kisha makubaliano yatakamilika,ni karibu..."

Aliongeza; "Filip tayari amekubaliana na masharti ,anataka kujiunga na Chelsea..ni suala la muda tu kumaliza kila kitu."

Chelsea kuingia sokoni kumtafuta kipa mpya inakuja baada ya madai kuwa Kepa Arrizabalaga huenda akaondoka klabuni humo.Kepa amekuwa Real Madrid kwa mkopo na huenda ujuzi wake haumvutii mkufunzi mpya Enzo Maresca.

Na je Filip Jorgensen ana ujuzi  upi?

 

Filip Jorgensen mwenye umri wa miaka 22 ni miongoni mwa kipa ambao wameonyesha ubabe wao msimu jana.

Ingawa alifungwa mabao 65 na kuweka 'clean sheet' sita pekee katika msimu wa 2023/24, Villarreal wangenyeshewa mvua ya mabao msimu jana kama Jorgensen hangekuwa michumani.

Kiwango cha pasi cha mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 kilikuwa muhimu kwa Villarreal katika kipindi chote cha kampeni za 2023/24, akikamilisha zaidi ya pasi 1,000 na wastani wa pasi 44.7 za mafanikio kwa kila dakika 90 akiwa na klabu yake.

Kwa kuzingatia mtindo wa kucheza wake  meneja mpya Enzo Maresca,ambao mara nyingi ni kumiliki mpira  na kupiga pasi mingi kutoka nyuma hadi mbele,Jorgensen huenda akawa jawabu kwa kocha huyo.

Kwa kuwa hakuna aliyekamilika,Jorgensen  ana mapungufu kama vile ku'command' wachezaji akiwa ugani. Vile vile anatatizika kuzuia mipira   ya hikabu hii inadhihirika kweli kwa kuwa alisimamisha 5.2% tu ya krosi zilizoingia kwenye kisanduku chake akiwa Villarreal.

Baada ya mechi ya hivi majuzi ya kujiandaa kwa msimu dhidi ya Wrexham, Maresca alisifu uchezaji wa Sanchez lakini aliacha mlango wazi kwa usajili zaidi, akisema.

"Kwa hakika, jinsi tunavyotaka kucheza, kipa ni muhimu sana - moja ya nafasi kuu."

Huku mustakabali wa Petrovic katika klabu haujulikani, nyongeza kama Jorgensen inaweza kutoa ushindani na ubora unaohitajika kwenye lango.