'Ni pre-season tu!' Sajili mpya Renato Veiga awapa moyo mashabiki wa Chelsea

Mashabiki wengi wa Chelsea wamejawa na hofu huku maswali mengi yakijaa akilini iwapo mambo yataboreka au la.

Muhtasari

•Chelsea iliambulia sare ya 2-2  kwenye  mechi ya kwanza ya kirafiki dhidi ya Wrexham kabla ya kupararishwa kwa kichapo cha kelbu msikitini na Celtic  4-1 .

•Kwa sasa mechi nne za kirafiki zimesalia,wakitarajiwa kucheza na Club America,Real Madrid,Manchester City na Inter Milan kabla ya ligi  kuu kuanza.

Renato Veiga
Image: Facebook

Sajili mpya wa Chelsea,Renato Veiga amewataka mashabiki wa Chelsea kuwa watulivu licha ya kuanza vibaya kwa The Blues kwenye mechi za kirafiki.

Kocha mpya Enzo Maresca alianza kwa chini  hii ni baada ya  sare ya 2-2 dhidi ya Wrexham  na kisha baadaye akalipuliwa  mabao 4-1 kutoka kwa Celtic na kuwaacha mashabiki wakiwa na wasiwasi kuhusu siku zijazo.

Kwenye mazungumzo na waandishi wa habari,Veiga anaamini hakuna sababu ya kuwa na wasiwasi katika hatua hii ya awali ya umiliki wa Maresca.

"Bila shaka ni kuhusu matokeo na katika kila mchezo wa soka unataka kushinda.Chelsea haswa inapaswa kushinda kila mechi. Lakini tuko katika maandalizi ya msimu mpya. Jambo muhimu zaidi ni mchakato, uhusiano kati ya kila mmoja."

Aliongeza; "Wakati ukifika Agosti 18 [dhidi ya City], hapo ndipo inapofaa na tunapolazimika kushinda kwa uhakika."

Akimzungumzia kuhusu kocha Maresca alisema;

"Ni meneja ambaye lazima ujue kile anachotaka ...yuko wazi kwa hakika. Lazima tu ufurahie na ujifunze kiwango cha juu unachoweza katika kila kipindi cha mafunzo, kutoa kila kitu unachoweza katika kila kikao - hiyo ni muhimu sana kwake kama vizuri na baada ya  hapo unaweza kuiga ."

 Hata hivyo, kiungo huyo ambaye ana uwezo  wa kucheza vizuri kama beki wa kati na beki wa kushoto, aliendelea kukiri kuwa bado hajui kama atabaki kwenye kikosi cha Maresca au atatolewa kwa mkopo msimu ujao.

"Tutaona mwishoni mwa msimu wa kabla ya msimu au baada ya soko kufungwa... Ninahisi imani kutoka kwa meneja na wafanyakazi wenzangu. Nataka tu kufanya kila niwezalo na tutaona bila shaka," alidai.

Chelsea wana mechi nne za kirafiki zilizosalia  kabla ya ligi kuu ya Uingereza kuanza.Wana mechi dhidi ya Club America,Manchester City, Real Madrid na kisha  Inter  Milan.

Katika mechi yao ya ufunguzi ya ligi kuu ya Uingereza watamenyana na mabingwa watetezi,Manchester City Agosti 18,2024.