Kocha mkuu wa Chelsea Enzo Maresca amepuuza ulinganisho kati yake na meneja wa Manchester City Pep Guardiola.
The Blues walimenyana na Cityzens mjini Columbus kama sehemu ya ziara zao za kabla ya msimu mpya nchini Marekani Jumamosi usiku ambapo walipoteza 4-2.
Maresca amesimamia mechi tatu za kirafiki tangu achukue kibarua cha Chelsea.
Walifungwa 2-2 na timu ya League One Wrexham kabla ya kufungwa 4-1 na mabingwa wa Uskoti Celtic, ingawa waliweza kuokolewa mapema wiki hii kwa ushindi mzuri wa 3-0 dhidi ya miamba wa Mexico Club America.
Katika mkutano wake na waandishi wa habari kabla ya mechi, Maresca, ambaye hapo awali alifanya kazi chini ya Guardiola akiwa City, aliulizwa kuhusu kufanana na tofauti kati yake na kocha huyo wa Kikatalani.
"Ningependa kuwa na nywele ndefu na macho ya bluu, na mke wangu labda anafikiria vivyo hivyo, lakini ikiwa watu wanataka kufanya ulinganisho siwezi kuwazuia," Maresca alisema.
"Tofauti ni kwamba yeye ndiye meneja bora zaidi duniani na mimi ni mmoja tu wa mameneja wengine."
Katika mahojiano na Daily Mail, Maresca alitoa jibu kama hilo alipoambiwa kwamba mara nyingi anaitwa kocha ambaye anajaribu kuwa kama Guardiola.
"Ni jambo la kuudhi? Hapana. Kwa sababu mwisho, nina mke wangu, nina watoto wangu, nina familia yangu. Sote ni tofauti," alijibu.
"Nilipojiunga na Chelsea, [Guardiola] alikuwa na furaha sana kwa sababu ana uhakika [kwamba] kwa muda, tunaweza kujenga kitu muhimu. Ikiwa niko hapa nilipo, ni kwa sababu yake."
Mechi ya kwanza ya ushindani kwa Maresca kama kocha wa Chelsea atakutana na City ya Guardiola katika uwanja wa Stamford Bridge wikendi ya ufunguzi wa msimu mpya wa Premier League.