Chelsea: Enzo Maresca amshtumu mtangulizi wake Pochettino kwa matatizo kwenye safu ya ulinzi

Maresca alidai kwamba timu yake inapitia changamoto kubwa kwenye safu ya ulinzi kutokana na mtindo wa kucheza uliachwa na Pochettino aliyeondoka mwishoni mwa msimu jana.

Muhtasari

• Walibebeshwa gunia la mabao 4 na Celtic ya Uskoti, kabla ya Man City pia kuwachabanga mabao 4-2 na Real Madrid kumaliza udhia kwa kuwapiga 2-1.

Pochettino na Maresca
Pochettino na Maresca

Kocha mpya wa klabu ya Chelsea Enzo Maresca ametupa lawama za kuvuja kwa safu ya ulinzi ya timu hiyo kwa mtangulizi wake Mauricio Pochettino. 

Chelsea ilifungwa zaidi ya mabao 60 kwenye ligi ya premia msimu uliopita na kocha mpya sasa anadai timu yake iko mbali sana kutoka kwa kupata uimara katika safu yake ya ulinzi.

Chelsea, chini ya Maresca walishiriki jumla ya mechi 5 za kujifua kuelekea msimu mpya nchini Marekani ambapo walipata ushindi mmoja, sare moja na vipigo 3.

Walibebeshwa gunia la mabao 4 na Celtic ya Uskoti, kabla ya Man City pia kuwachabanga mabao 4-2 na Real Madrid kumaliza udhia kwa kuwapiga 2-1.

Maresca alidai kwamba timu yake inapitia changamoto kubwa kwenye safu ya ulinzi kutokana na mtindo wa kucheza uliachwa na Pochettino aliyeondoka mwishoni mwa msimu jana.

Alisema; "Moja kati ya masuala yangu katika mkutano wa kwanza na timu ilikuwa kuhusu idadi ya mabao tuliruhusu kufungwa mwaka jana na safu ya ulinzi ikiwa imefurika. Sisi hatutaki kutumia safu ya ulinzi kubwa, hiyo ni tabia ya msimu jana, ama miaka iliyopita, sijui."

"Tumajaribu kutanua kidogo safu ya ulinzi, angalau kwa mita 4 au 5 ili kuwa na nafasi nzuri. Mwaka jana tayari tulifungwa mabao mengi na hilo tattoo. Nina imani tunaweza litatua hivi karibuni," aliongeza.