Kwanini Samu Omorodion alikataa ofa ya Chelsea ‘isiyo na heshima’ na kuvunja mazungumzo

Metrok UK wanaripoti kwamba Kulingana na El Chiringuito, mzozo huo ulihusu hamu ya Chelsea kununua asilimia 50 ya haki za picha za Omorodion.

Muhtasari

• Metrok UK wanaripoti kwamba Kulingana na El Chiringuito, mzozo huo ulihusu hamu ya Chelsea kununua asilimia 50 ya haki za picha za Omorodion.

SAM OMORODION
SAM OMORODION

Mshambulizi wa Atletico Madrid Samu Omorodion alikataa kuhamia Chelsea kutokana na kutofautiana kuhusu haki za picha, kulingana na ripoti nchini Uhispania, kwa mujibu wa jarida la Uingereza, Metro UK.

Chelsea walionekana kukaribia kumsajili Omorodion baada ya kuafikiana na Atletico Madrid kwa kitita cha Euro milioni 40 (£34.5m).

Hata hivyo, uhamisho wa Omorodion kwenda Stamford Bridge uliporomoka wikendi kwa sababu mshambuliaji huyo hakuweza kufikia makubaliano kuhusu masuala ya kibinafsi.

Metrok UK wanaripoti kwamba Kulingana na El Chiringuito, mzozo huo ulihusu hamu ya Chelsea kununua asilimia 50 ya haki za picha za Omorodion.

Ripoti hiyo inadai kuwa Omorodion anahisi Chelsea imeonyesha kutoheshimu pendekezo lao na kwa sababu hiyo, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 hayuko tayari kufanya mazungumzo yoyote.

Omorodion, ambaye alifunga mabao nane katika mechi 35 wakati wa kipindi chake cha mkopo akiwa na Alaves msimu uliopita na kushinda medali ya dhahabu ya Olimpiki akiwa na timu ya soka ya wanaume ya Uhispania msimu huu wa joto, sasa anatarajiwa kusalia Atletico.

Chelsea sasa wameelekeza nguvu zao kwa kumsajili tena Joao Felix kutoka Atletico.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, ambaye alitumia miezi mitano kwa mkopo Chelsea mwaka jana, tayari ameonyesha kuwa yuko tayari kurejea Stamford Bridge kwa kipindi cha pili.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno alicheza kwa mkopo Barcelona msimu uliopita, na kufunga mabao 10 katika mechi 44.

Akizungumza mwezi Juni, rais wa Barcelona, ​​Joan Laporta, alidai kuwa kocha mkuu mpya wa klabu hiyo, Hansi Flick, alikuwa na nia ya kumbakisha Felix Camp Nou.