logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Timu ya Chelsea kumpa Nicolas Jackson mkataba ulioboreshwa

Chelsea imempa donge nono mshambulizi Jackson

image
na Davis Ojiambo

Michezo14 August 2024 - 13:04

Muhtasari


  • •Chelsea imempa donge nono mshambulizi Jackson .
  • •Mshambulizi Nicolas Jackson kuongeza mkataba na timu ya Chelsea
Chelsea.

Klabu ya Chelsea inayoshiriki ligi kuu ya uingereza, sasa iko radhi kukubali mshambuliaji wao Nicolas Jackson atie sahini mpya baada yakua wameridhia na mchezo hasa katika safu ya uvamizi.

Aidha Jackson atapata nyongeza ya mshahara na kupata fursa zaidi ya kuchezea timu hiyo msimu hujao.

Hii inakuja siku chache baada ya kinda wa timu hiyo Cole Palmer kuongeza mkataba wake hadi mwaka 2033.

Mshambulizi huyo alifanya vyema katika michuano yote huku akichangia pakubwa upatikanaji wa mabao.

Chelsea inatarajiwa kufanya msimu huu uku kocha wao mpya Enzo Maresca akiipigia upatu mkubwa timu hiyo licha ya kuandikisha matokeo duni katika michuano ya kirafiki kwa ajili ya msimu mpya utakaoanza mwishoni mwa wiki hii.

Mazungumzo baina ya bodi ya Chelsea na Jackson yameanza ambapo nduru za kuaminika zina ashiria kua yupo tayari kwa mkataba mpya na timu hiyo ya Chelsea .





RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved