Pep Guardiola amsifia kiungo Rico Lewis

Kocha wa mabingwa watetezi Manchester City asema amefurahishwa na mchezo wa inda Rico Lewis.

Muhtasari

•Pep Guardiola amesifia Rico Lewis ambaye ameonyesha tajiriba kubwa katika safu ya ulinzi na utengenezaji nafasi za mabao.

RICO LEWIS
RICO LEWIS
Image: RICO LEWIS//MANCHESTER CITYFACEBOOK

Kocha wa klabu ya Manchester City ambao ni mabingwa watetezi wa ligi kuu Uingereza Pep Guardiola amesema kuwa Rico Lewis ni mchezaji bora.

Kinda  huyo nayecheza kama kiungo mkabaji  alitokea akademia ya timu  hiyo na kuwa kiungo muhimu huku akivalia jezi  nambari 82.

Baada ya timu ya City kuilabua Chelsea mabao mawili kavu, katika mechi ya ufunguzi,Pep alimsifia sana Lewis akisema amependezwa namna  alicheza katika safu ya ulinzi .

Aidha ,Lewis ni mchezaji mwenye uzoefu katika nafasi ya ulinzi pande zote mbili ,na ambaye aliiongoza timu ya Manchester city U18 akiwa na umri wa miaka 15 kuonyesha umahiri katika taaluma ya kusakata soka huku wakishinda taji hilo 2018.

Msimu wa 2022-23, Lewis alijumuishwa katika kikosi cha kwanza timu ya City na ambapo alianzishwa katika timu ya kwanza na kupachipika bao walipokuwa wakicheza na Sevilla katika kombe la maskio marefu.

Lewis, ambaye alitia mkataba wake wa miaka mitano mwaka jana amekuwa na ubora wake akiichezea timu hiyo ya City ambapo wameshinda mataji ikiwemo kombe kuu la ligi ya Uingereza mara nne mfululizo.

Kando na timu ya City ,Lewis ameichezea timu ya taifa ya Uingereza U18 na kucheka na wavu mara moja.Lewis amefunga mabao 3 katika taaluma yake.