Mshambuliaji João Felix arejea Chelsea, mkataba wa miaka sita

Mreno João Felix kutoka klabu ya Atlético Madrid arejea Uingereza kwa mkataba wa miaka sita.

Muhtasari

•Mreno João Felix arejea klabu ya Chelsea kwa mkataba wa kudumu kwa kipindi cha miaka 6,baada ya kutarajiwa kufanya vipimo vya kiafya hii leo ili kuisaidia timu hiyo kujikwamua baadaya kusuasua kwa mda.

JOAO FELIX//FACEBOOK
JOAO FELIX//FACEBOOK
Image: JOAO FELIX//FACEBOOK

Mreno João Felix ,24, kutoka klabu ya Atlético Madrid, sasa amekubali kujiunga na klabu ya Chelsea kutoka ligi kuu nchni Uingereza kwa mkataba wa miaka 6.Felix alikua akiichezea timu ya The Blues lakini kwa mkopo kutoka timu  ya Barcelona alipokuwa akichezea timu hiyo kwa mkopo, baada ya kucheka na nyavu mara kumi na kuchangia migongeo sita iliyozalisha mabao.

Felix atakua anajiunga na klabu hiyo ya Chelsea baada kukamilisha uhamisho wake ,ambapo vipimo vya afya vinatarajiwa kufanywa hii leo, ili kujiunga na kikosi hicho cha Enzo Maresca rasmi .

Felix alianza taaluma yake katika klabu ya Benfica, na amekua nguzo kubwa hasa akiichezea Ureno katika hatua za kitaifa na kuchangia kupatikana kwa mabao.

Baadhi ya mashabiki wa Chelsea wamefurahishwa na sajili la kinda huyo hasa ikikumbukwa alichangia pakubwa katika klabu hiyo wakati alikua mkopo kabla kwenda zake.Aidha Felix katika msimu wa 2022-23 ,alionekana kuwa mwiba  katika klabu hiyo ya Chelsea baada kufunga mabao 4, licha ya kipindi kifupi alipohudumia vijana hao wa The Blues.

Felix anatarajiwa kujumuishwa katika mechi ifutayo ili kuwania taji la ligi kuu Uingereza baada ya timu hiyo Chelsea kupteza mechi ya ufunguzi dhidi ya Man City.