Mlinda lango Manuel Neur astaafu kuchezea timu ya Taifa ya Ujerumani

Kupitia ukurasa wake rasmi wa Facebook ,Neur aliandika kuwa,"baada ya zaidi ya miaka 15,na kuoneka mara 124, katika timu ya Taifa,leo inatamatisha siku yangu mimi kuichezea timu ya Ujerumani ya kandanda".

Muhtasari

• Manuel Neur atangaza kustaafu kuchezea timu ya kandanda ya taifa ya Ujerumani baada ya kushiriki katika michuano mingi katika timu hiyo na kutofungwa mabao kwa mechi 51.

MANUEL NEUR
MANUEL NEUR
Image: MANUEL NEUR//FACEBOOK

Manuel Neur,mzawa wa Ujerumani na ambaye alizaliwa tarehe 27 machi ,mwaka wa 1986,sasa amestaafu kuchezea timu hiyo ya Taifa baada ya kucheza michuano 124 na kusaidia timu hiyo ya Ujerumani kushinda mataji mbali mbali ikiwemo kombe la UEFA European cup mwaka wa 2009,kwa wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21.

Kupitia ukurasa wake rasmi wa Facebook ,Neur aliandika kuwa,"baada ya zaidi ya miaka 15,na kuoneka mara 124, katika timu ya Taifa,leo inatamatisha siku yangu mimi kuichezea timu ya Ujerumani ya kandanda". 

Neur, ambaye kwa sasa anaichezea timu ya Bayern Munich  inayoshiki katika ligi kuu ya Ujerumani ,amekuwa kiungo muhimu,hasa akiwa golikipa ambaye anauzoefu na tajriba kibao kataka kikosi hicho.

Neur ,Aidha ,ameisaidia timu hiyo ya Bayern Munich kushinda mataji si haba akiwa mlinda lango .Vilevile, Neur ameweza kutuzwa mataji mengi kama golikipa akiwa mchezaji ujanani na akiwa na umri mkubwa.

Golikipa huyo aliisaidia timu hiyo ya taifa ya Ujerumani kumaliza katika nafasi ya  tatu katika  kombe la Dunia  2014.

Kupitia ukurasa wa Facebook wa timu ya Tifa,wamemshukuru sana Neur kwa uongozi wake na vilevile kuwapa wachezaji chipukizi hasa magolikipa motisha na kuiga nyayo zake.