"Napenda mchezo wa Madueke" : Enzo Maresca

Kocha wa klabu ya Chelsea amesema kuwa amefurahaishwa na mchezo wa Noni Madueke.

Muhtasari

• Maresca amesema kuwa amekubali mchezo wake na yuko tayari kumuweka kikosini kwa huduma za usoni,"nataka kumweka kwa ajili ya siku zijazo".

NONI MADUEKE
NONI MADUEKE
Image: NONI MADUEKE//FACEBOOK

Kocha wa klabu ya Chelsea ,Enzo Maresca amesema kuwa anapenda mchezo wa wing'a Noni Madueke.

Kauli hii inajiri baada ya The Blues kushinda katika pambano la Europa Conference League  play-off mkondo wa kwanza dhidi ya  Servette mabao 2-0.

Maresca  alisema kuwa "Napenda mchezo wa Noni Madueke..lakini shida kubwa yake ni lazima afanye mazoezi kwa mfululizo" 

Aidha Maresca amesema kuwa amekubali mchezo wake na yuko tayari kumuweka kikosini kwa huduma za usoni,"nataka kumweka kwa ajili ya siku zijazo".

Mabao ya Chelsea yalipatikana kupitia wachezaj Christopher Nkunku kupitia mkwaju wa penalti naye Noni Madueke akaongeza la pili na kusaidia vijana hao wa Enzo kusajili ushindi muhimu wakiwa nuymbani na sasa wanasubiri mechi ya marudio.

Sarvette FC timu inayoshiriki ligi ya Uswizi na watakuwa wenyeji wa timu hiyo ya kutoka Uingereza katika mkondo wa pili katika michezo hiyo ya Uefa Conference League.

Madueke ,ambaye amekuwa akisaidia timu hiyo ya Chelsea katika ufungaji mabao,alianza taalima yake katika klabu ya Uholanzi PSV Eindhovein.Mzawa huyo wa Uingereza ameichezea timu ya Uingereza u21 na kushinda taji la Europa 2021.

Madueke anatarajiwa kutamba msimu huu baada ya kudhihirisha uwezo wake alipoanzishwa katika mechi kadhaa chini ya ukufunzi wake Pochettino.