Kombe la CAF: Gor na Police FC zasonga baada ya ushindi muhimu

Timu za hapa kenya zinazoshiriki katika ligi kuu ya KPL zimepiga hatua katika hatua nyengine mashindano ya CAF .

Muhtasari

•Timu mbili  zinazoshiriki katika ligi kuu KPL, sasa zimepiga hatua katika kombe la CAF ,baada ya kupata ushindi kunako siku ya jana.

•Gor Mahia,waliinyuka timu ya Al Merreikh ya Sudan kusini mabao 5-1 na kuwabandua nje kwa jumla ya mabao 5-2.

MCHEZAJIWA KENYA POLICE NA MASHABIKI WA KOGALO
MCHEZAJIWA KENYA POLICE NA MASHABIKI WA KOGALO
Image: PICHA KWA HISANI

Timu za Gor mahia na ile ya Kenya Police zimetinga katika hatua  nyengine kushiriki katika hatua ya kwanza katika kombe la CAF champions League, kutokana na ushindi ambao timu hizo zilipata siku ya Jumapili.

Mechi ya Gor ya raundi ya pili ilichezwa hapa nyumbani nchini Kenya na Police fc walichezea ughaibuni, Uhabeshi.

Katika raundi ya kwanza,Gor Mahia  walipokuwa wakicheza na timu ya Al Merreikh ya Sudan kusini ugenini walishindwa kwa ushindi mkonde wa bao 1-0.

Hata hivyo, walirekebisha mambo katika mechi ya mrudiano iliyogaragazwa ugani Nyayo,na kupata ushindi mkubwa wa mabao 5-1 na kusonga mbele katika kombe hilo .

Timu ya Kenya Police kwa upande wao walipata ushindi wakicheza na timu ya Ethiopia Coffee Sc na kuibuka na ushindi wa 1-0.

Kufuatia ushindi huo, Gor Mahia watecheza na washikilizi rekodi katika utwaaji wa kombe hilo, kutoka Misri, Al Ahly SC, na ambapo mkondo wa kwanza utachezwa tarehe 13  septemba mwaka huu na kisha baadae mrudiano mwezi huo huo tarehe 20 .

Kenya Police watachuana na mabingwa watetezi Zamalek hapa nyumbani tarehe 13  septemba mwaka huu na kisha baadae mrudiano mwezi huo huo tarehe 20 .