Wachezaji wa Real wataondoka uwanjani kwa sababu ya ubaguzi wa rangi - Vinicius Jr

"Tunahitaji kuondoka uwanjani ili mambo yabadilike haraka iwezekanavyo," Vinicius alisema.

Muhtasari

•Vinicius Jr amesema yeye na wachezaji wenzake wataondoka uwanjani iwapo watakabiliwa na ubaguzi wowote wa rangi msimu huu.

•"Vinicius Jr alisema njia pekee ya kuondosha ubaguzi wa rangi kwenye soka kabisa inaweza kuwa kwa kusimamisha mechi.

Image: BBC

Mshambuliaji wa Real Madrid Vinicius Jr amesema yeye na wachezaji wenzake wataondoka uwanjani iwapo watakabiliwa na ubaguzi wowote wa rangi msimu huu.

Fowadi huyo wa Brazil alizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mapema mwaka huu alipozungumza kuhusu unyanyasaji ambao amekumbana nao, akisema anahisi "kuisha kwa hamu ya kucheza kandanda.

Na sasa Vinicius Jr anasema Real itaondoka uwanjani ikitaka msimu huu.

Aliiambia CNN:, external "Tunahitaji kuondoka uwanjani ili mambo yabadilike haraka iwezekanavyo.

"Mashabiki watatu wa Valencia hivi majuzi walihukumiwa kifungo cha miezi minane jela kwa kosa la kumtusi nyota huyo kwenye mechi ya tarehe 21 Mei 2023.

Mashabiki hao walipatikana na hatia ya "uhalifu dhidi ya uadilifu wa maadili" na "hali inayozidisha ya ubaguzi kulingana na nia za kibaguzi.

"Vinicius Jr alisema njia pekee ya kuondosha ubaguzi wa rangi kwenye soka kabisa inaweza kuwa kwa kusimamisha mechi.

"Katika kilabu, tunazungumza juu yake mara nyingi," alisema mchezaji huyo wa miaka 24. "Siyo mimi tu, lakini wachezaji wote walisema kama hilo likitokea, wakati mwingine kila mmoja atalazimika kuondoka uwanjani. Ili wale wote waliotutusi walipe adhabu kubwa zaidi.