Sajili mpya wa Arsenal Mikel Merino apata jeraha hata kabla ya kuwachezea mechi moja

"Bahati mbaya sana," Arteta alisema. "Jana aligongana na Magalhaes na ana jeraha la bega kwa bahati mbaya. Inaonekana atakuwa nje kwa wiki chache.”

Muhtasari

• Kiungo huyo alikuwa amekamilisha tu uhamisho wake kutoka Real Sociedad Jumanne na angetarajia kucheza mechi yake ya kwanza Arsenal dhidi ya Brighton Jumamosi.

MIKEL; MERINO.
MIKEL; MERINO.
Image: X

Arsenal imepata pigo kubwa baada ya mchezaji mpya aliyesajiliwa kwa pauni milioni 31.6 Mikel Merino kuumia bega katika mazoezi yake ya kwanza akiwa na timu hiyo.

Merino alijeruhiwa bega katika mazoezi siku ya Alhamisi na meneja wa Arsenal Mikel Arteta amethibitisha kuwa kiungo huyo atakuwa nje kwa "wiki"

Kiungo huyo alikuwa amekamilisha tu uhamisho wake kutoka Real Sociedad Jumanne na angetarajia kucheza mechi yake ya kwanza Arsenal dhidi ya Brighton Jumamosi.

Lakini sasa Merino lazima asubiri na anatarajiwa kufanyiwa uchunguzi zaidi huku Arsenal wakitafuta kujua kiwango kamili cha jeraha lake.

"Bahati mbaya sana," Arteta alisema. "Jana aligongana na Magalhaes na ana jeraha la bega kwa bahati mbaya. Inaonekana atakuwa nje kwa wiki chache.”

“Kikao cha kwanza. Alifurahi sana na kila kitu kilikuwa kizuri sana. Alitua sakafuni na Gabi [Magalhaes] akatua juu yake na inaonekana kana kwamba ana mpasuko mdogo pengine.

"Lazima tuone [atakuwa nje kwa muda gani]. Alikuwa na maumivu makali sana. Itabidi tufanye majaribio zaidi juu ya hilo kisha tutakuwa na majibu ya kuhitimisha zaidi.

Arsenal pia watamkosa Gabriel Jesus katika mchezo wa Jumamosi dhidi ya Brighton baada ya kupata jeraha la paja wiki iliyopita.