•Timu ya AFC Bournemouth yawa yakwanza katika historia ya ligi kuu Uingereza ,kusawazisha mabao mawili na kupata ushindi baada ya dakika 87.Bournemouth,walipata ushindi wa mabao matatu kwa mawili wakicheza na timu ya Everton ugenini na kunyakuwa alama zote tatu.
Timu inayoshiriki katika ligi kuu nchini Uingereza ya AFC Bournemouth,sasa imekuwa timu ya kwa kuwai kutokea kupata ushindi huku wakiwa chini mabao mawili kunako dakika ya 87.
Bournemouth ,walipata ushindi wao wakiwa ugenini walipokuwa wakicheza na timu ya Everton.
Everton ambao walikuwa wenyeji wa Bournemouth,walipata mabao yakuongoza kupitia wachezaji Calvert-lewin na M. keane na kudhania kuwa wameweka alama zote mfukoni, jambo ambalo liliwafanya kujisahau na kuzembea.
Bournemouth,walirejea mchezoni ,baada ya mchezaji Semenyo kupata bao kunako dakika ya 87, kutokana na mashambulizi ya klabu hiyo katika dakika za nyongeza ,iliweza kurejesha bao la kusawazisha kupitia mchezaji Lewis Cook,na baadae kupata la ushindi kupitia mchezaji Sinisterra.
Mechi hiyo ambayo ilitamatika kwa mabao 2-3 na kupelekea timu hiyo kuwa ya kwanza kushinda wakiwa chini mabao mawili kufikia dakika ya 87 na kurejea mchezoni na hatimaye kupata ushindi,na kuweka pointi zote tatu kibindoni wakiwa ugenini.
Bournemouth ,ambao kwa sasa wameshikilia katika nafasi ya nane katika msimamo wa jedwali la ligi kuu Uingereza baada ya mechi tatu kugaragazwa wakiwa na pointi 5.
Bournemouth watakuwa wanawaalika vijana wa Chelsea tarehe 14 septemba katika uga wa Vitality Stadium.