Ni kichapo 'kisichokubalika' - Virgil van Dijk azungumzia matokeo dhidi ya Nottingham

Nahodha huyo alisema kuwa kipigo hicho kitakuwa kichocheo cha kushinda mechi ya klabu bingwa ulaya.

Muhtasari

•Beki wa klabu ya Liverpool,Virgil van Dijk alisema kuwa kichapo cha bao moja kavu na Nottingham Forest,ni 'mafuta' ambayo yatawafanya kupiga klabu ya Ac Milan,kombe la mabingwa ,jumanne 17.

•Bao lake Calum Hudson-Odoi,lilikuwa tosha kusambaratisha msururu wa kutopoteza mechi nyumbani.

VIRJIL VAN DIJK//FACEBOOK

Kufuatia kichapo cha bao moja sifuri na klabu ya Nottingham Forest, sasa beki wa Liverpool na Uholanzi Virgil van Dijk, amesema kuwa Liverpool lazima walitakase jina lao baada ya kibano hicho 'kisichokubalika' wakiwa nyumbani Anfield.

Nahodha huyo alisema kuwa kipigo hicho kitakuwa kichocheo cha kushinda mechi ya klabu bingwa ulaya.

Historia ya kutoshindwa wakiwa nyumbani ya The Reds ilivunjwa siku ya Jumamosi 13,2024 baada ya muda mrefu na timu ya Forest.

Bao lake aliyekuwa mchezaji wa Chelsea Calum Hudson- Odoi,l ilikuwa tosha kwa klabu hiyo kunyakuwa pointi zote tatu wakiwa ugenini.

Aidha, van Dijk alisema sasa klabu hiyo lazima itakase jina kwa sasa wakiendelea kufanyia maozoezi kombe la mabingwa huku wakifungua udhia na klabu ya Ac Milan,Jumanne 17.

Liverpool,ambao walipata ushindi katika mechi zake za kwanza tatu na baadae kupigwa na Forest,kibano ambachowengi hawakutarajia.

van Dijk,alisema kuwa kikosi cha liverpool hakina budi ila tu kushinda pambano hilo la kombe la mabingwa dhidi ya Ac Milan.Aidha,alisema kuwa kikosi chote kinaelewa kuwa kushindwa kwao ni jambo ambalo kwao hawakutarajia na ni jambo ambalo hawawezi kukubali kiurahisi.

Vile vile,nahodha  huyo alisema kuwa kuwa wanahitaji huduma za kila mchezaji ili kuhakikisha kwamba watasajili matokeo ya kuridhisha .

Van Dijk,alisema vile vile inafurahisha kwa kuwa wamerudi katika kombe hilo la mabingwa ,"klabu kama Liverpool inahitaji kuwa kwenywe kombe la mabingwa ,na  kwasasa tumerejea na matokeo ambayo ni ya kuridhisha na pia mchezo mzuri kwa mtazamo wangu ,ni ule ambao unahitajika hili kucheza hapa"