Victor Olatunji awa mchezaji wa 2 Afrika kufunga na kutoa pasi katika mechi ya kwanza Champions League

Mchezaji Victor Olatunji mzawa wa Nigeria awa mchezaji wa tatu Afrika kupachika bao na kutoa pasi iliyozalisha bao katika kombe la Champions League akiichezea Sparta Prague.

Muhtasari

•Victor Olatunji mzawa wa Nigeria amekuwa mchezaji wa tatu kupachika bao na kutoa mgongeo wa bao Afrika katika kombe la Champions League katika mechi ya kwanza.

•Aidha,Olatunji ni wa kwanza kwa taifa la Nigeria kupachika bao na kutoa pasi la bao katika mchuano mmoja,kombe la bingwa ulaya katika mechi yake ya kwanza.

VICTOR OLATUNJI
Image: HISANI

Mchezaji mzaliwa wa taifa la Nigeria anayechezea timu ya Sparta Prague inayoshiriki katika ligi kuu ya Czech Republic, Victor Olatunji mwenye miaka 25 sasa ameingia katika orodha ya wachezaji ambao washaapata bao na kuzalisha bao kwenye  mechi ya kwanza, kutoka  barani Afrika.

Olatunji, kwa sasa ni mchezaji wa tatu kufunga bao na kutoa pasi ya kuzalisha bao baada ya wachezaji Daniel Cousin aliyepachika bao na kutoa pasi ya bao mnamo 2007 mechi baina ya (Rangers na Lyon) na mchezaji Serge Aurier mnamo mwaka wa 2015 wakati PSG ikimenyana na Shakhtar Donetsk kwenye mechi yao ya ufunguzi.

Mshambuliaji huyo ambaye baada wa kuwa wa tatu Afrika ameongoza orodha hiyo huku akiwa wa kwanza kwa taifa hilo la Nigeria.

Olatunji ,alifunga bao kunako dakika ya 42 na kutoa pasi ya bao kunako dakika ya 58 kwa mchezaji Qazim Laci ambaye alipachika bao wavuni . Bao lake Olatunji, na mgongeo huo, aluwasaidia vijana hao wa Sparta Prague kupata ushindi mkubwa nyumbani wa mabao matatu kwa sifuri dhidi ya Rb Salzburg.

Olatunji aidha, alichaguliwa mchezaji bora wa pambano hilo jambo ambalo linaashiria kujituma kwa mshambuliaji huyo kinda.

Olatunji baada ya kufunga bao aliuiga mtindo wake Christiano Ronaldo 'siuuuuuuu' na ambapo alikuwa amevalia shati lilikokuwa na maandishi "I AM A CHOSEN, WHO ARE YOU'.