Rekodi ya Kylian Mbappé Monaco yavunjwa

George Ilenikhena avunja rekodi ya Kylian Mbappé katika klabu ya As Monaco na kuwa mchezaji mchanga zaidi kuwai kufunga kwenye Kombe la Mabingwa.

Muhtasari

•George Ilenikhena aivunja rekodi ya Mbappé ya kuwa mchezaji mchanga kuwai kutokea kufungia timu ya AS Monaco katika Kombe la mabingwa.

•George alifunga bao hilo kwa sasa akiwa na umri wa miaka 18 na siku 34 na kumpiku Kylian Mbappé aliyefungia timu hiyo akiwa na umri wea miaka 18 na siku 64.

•Bao lake Ilenikhena kunako dakika ya 71, liliisaidia timu hiyo ya AS Monaco kuilaza timu ya Barcelona 2-1 kwenye mechi ya hatua za makundi.

GEORGE//MBAPPE
Image: HISANI

George Ilenikhena amevunja rekodi ya Kylian Mbappé ya kuwa mchezaji mchanga kucheka na nyavu katika klabu ya Monaco ya Ufaransa katika kombe la klabu bingwa Ulaya.

George ambaye alifunga bao lake la kwanza katika michuano hiyo ana umri wa miaka 18 na siku 34, na kwa hivyo kuivunja rekodi ya Mbappé alifungia timu hiyo akiwa na umri wa miaka 18 na siku 64.

Ilenikhena,ambaye ni raia wa Nigeria, aliisaidia timu ya AS Monaco kuilaza timu ya Barcelona mabao mawili kwa moja katika mechi ya hatua za makundi kuwania taji la ligi ya mabingwa barani ulaya, alifunga kunako dakika ya 71.

Kufuatia ushindi huo,umekua wake wa kwanza katika kipute hicho na kuwafurahisha mashabiki wa nyumbani kwa ushindi huo mkubwa wakicheza na timu hiyo ya Uhispania.Mechi hiyo iligaragazwa tarehe 19, septemba.

Umekuwa mwanzo mzuri kwa mshambuiliaji huyo ambaye alitia wino na timu hiyo mnamo tarehe 25 julai.

Ilenikhena,ambaye anatambulika sana kwa kasi na chenga za maudhi,anacheza kama mshambuliaji wa katikati,amsesifiwa sana na kocha Philippe Hinschberger,akisema kuwa Ilenikhena ako na uwezo mkubwa sana ukizingatia anatumia guu lake la kushoto ambalo umsaidia kufanya ushambulizi wenye uzito.

Ilenikhena,ni mzawa wa Nigeria lakini akahamia Ufaransa kama mkimbizi na sasa amekuwa akijumuishwa kwa timu ya taifa ya wachezaji wachanga.