Shirikisho la soka barani Afrika CAF kupitia bodi ya nidhamu
imeaidhibu timu ya taifa la Libya baada ya mahangaiko iliyopitia timu ya
Nigeria nchini Libya.
Kupitia ujumbe kwa vyombo vya habari, bodi hiyo ya nidhamu baada
ya kufanuya uchunguzi iliipata Libya na makossa ya kukiuka vifungu vya 31, 82
na 151 vya sheria vya CAF.
Mataifa hayo mawili yalifaa kucheza mechi za kufuzu kombe ya
mataifa barani Afrika AFCON mnamo tarehe 15 October lakini mechi ilihairishwa
kutokana na upokezi mbovu wa timu ya Nigeria katika uwanja wa ndege nchini
Libya.
Kutokana na hatia, Nigeria wamefaidi magoli matatu na alama
tatu baada ya mechi hiyo kufutiliwa mbali na CAF.
Vile vile, shirikisho la soka la nchi ya Libya, limepigwa
faini ya dola elfu hamsini na imetakiwa kulipa faini hiyo chini ya siku sitini baada
ya kutaarifiwa na CAF.