logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Maseneta waonyesha wasiwasi wao kwa uchaguzi wa FKF utakaofanyika Desemba 7

Seneta wa Vihiga amesema kuwa uchaguzi huo tayari umeibwa kwa faida ya viongozi walio uongozini sasa

image
na Brandon Asiema

Football30 October 2024 - 16:17

Muhtasari


  • Seneta Mumma alitaka kamati ya leba na ustawi wa jamii ya bunge la seneti kutoa ripoti kuhusu utiifu wa kananu zinazosimamia shirikisho la soka nchini FKF na katiba ya Kenya.
  • Osotsi amesema kuwa bodi ya kusimamia uchaguzi huo iliteuliwa na viongozi walioko mamlakani kwa sasa hivyo basi matokeo ya uchaguzi huo huenda yakawa kinyume na matokeo halisi.

caption

Seneta wa Kaunti ya Vihiga Godfrey Osotsi amesema kuwa uchaguzi wa FKF unaotarajiwa kufanyika tarehe 7 Desemba tayari umeibwa.


Seneta Osotsi amesema hayo katika bunge la seneti mnamo Jumatano tarehe 30, akitoa maoni kuhusu kauli ya Seneta mteule Catherine Mumma kuhusiana na soka la nchini.


Kwa mujibu wa seneta Osotsi, kauli ya seneta Mumma imejitokeza kwa wakati unaostahili kwani sekta ya soka nchini itakuwa inafanya uchaguzi wake hivi Karibuni.


Osotsi amesema kuwa bodi ya kusimamia uchaguzi huo iliteuliwa na viongozi walioko mamlakani kwa sasa hivyo basi matokeo ya uchaguzi huo huenda yakawa kinyume na matokeo halisi.


“Uchaguzi huu tayari umeibwa kwa sababu ofisi ya sasa ndio iliteua watu watakaoendesha uchaguzi huo na kama hivyo ndivyo kulivyo basi matokeo yatakuwa kwa upendeleo wao.”  Alisema seneta Godfrey Osotsi.


Seneta huyo alisema kuwa uongozi wa sasa umewaangusha Wakenya katika kukuza soka la Kenya.


Seneta Osotsi pamoja na baadhi ya maseneta wengine wamesisitiza haja ya kuwepo kwa uongozi wa watu walio na tajriba kuendesha soka la humu nchini akisema kuwa tatizo linaloikumba sekta ya michezo nchini makampuni ambayo yamejiingiza katika soka, raga, riadha na michezo mingine.


“Hii nchi ina uwezo wa kufanya vyema katika michezo haswa kabumbu lakini kwa sababu tumeruhusu watu wasio na uelewa wa soka kuendesha sekta hiyo ndio wanasimamia soka.”   Aisema Osotsi.


Awali, seneta Mumma alitaka kamati ya leba na ustawi wa jamii ya bunge la seneti kutoa ripoti kuhusu utiifu wa kananu zinazosimamia shirikisho la soka nchini FKF na katiba ya Kenya.



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved