Mathare United imewaadhibu wake wanne kwa utovu wa nidhamu
baada ya kukiuka sheria ya mkataba baina yao na klabu hiyo.
Klabu hiyo imeafikia kuwachukulia hatua ya nidhamu wachezaji
Kevin Kimani, Elli Asieche, Brian Ouru na Eric Mulu baada ya kushiriki katika mashindano mengine
wakichezea timu nyingine bilaya rukhusa ya klabu walioweka mkataba nao.
Taarifa ya usimamizi wa Mathare United imesema kwamba wane hao
walichezea timu nyingine ambayo haijatajwa kabla ya Mathare kucheza mchuano wao
wa sita wa ligi dhidi ya Police FC.
Wachezaji waliopatikana na utovu wa nidhamu wameadhibiwa
kukosa mshahara wa wiki mbili kuanzia Jumatano ya tarehe 30, Oktoba.
Uamuzi wa mwisho wa Mathare United kuhusu swala hiyo
umetolewa timu hiyo ikisema kuwa wachezaji hao walivunja vipengee kadhaa katika
mkataba ikiwemo kukosa kuweka viwango
vya juu vya ubora wa mwili wakati wote.
Vile vile usimamizi wa Mathare United umesema
kuwa wachezaji hao walikiuka mkataba kwa kushiriki katika michezo mingine
inayoweza hatarisha ubora wa mili yao.