Kocha anayeondoka Sporting CP Ruben Amorim alisherehekewa wa
wachezaji na makocha wengine waliohudumu chini yake katika klabu hiyo baada ya
mechi yake ya mwisho katika klabu hiyo.
Amorim anatarajiwa kujiunga na klabu ya Manchester United tarehe 11 Novemba baada ya makubaliano ya kumuajiri kazi kuafikiwa baina ya Man United na Sporting CP kwa Man U kulipa Yuro milioni 10 kupata huduma za Amorim.
Katika mechi yake ya mwisho akiongoza Sporting CP, Amorim alishinda mechi hiyo ya klabu bingwa barani Ulaya kwa kuicharaza Manchester City mabao manne kwa moja.
Ushindi huo ulimpa kwaheri nzuri akitoka Ureno kuelekea Uingereza anakokwenda kuongoza mojawapo wa klabu kubwa duniani ya Manchester United.
Amorim anajiunga na Manchester United baada ya kutimuliwa kwa kocha Erik Ten Hag kutokana na matokeo mabovu chini ya umeneja wake.
Amorim tangu kujiunga na Sporting CP miaka mine iliyopita
ametwaa mataji mawili ya ligi kuu nchini Ureno.
Aidha akizungumza na wanahabari baada ya kulazwa mabao manne, kocha Pep Guardiola amesifia kocha Amorim kwa ushindi wao akisema kuwa hakika Amorin alistahili ushindi huo kutokana na mchezo mzuri waliocheza