logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Zaidi ya timu 200 kushiriki kinyang'anyiro cha Sakaja Super Cup

Mechi zimepangwa kuchezwa Jumamosi na Jumapili wiki hii huku jila kaunti ndogo ikitarajiwa kuwa na timu zisizozidi nane.

image
na Tony Mballa

Football12 November 2024 - 18:48

Muhtasari


  • Mabingwa watetezi, Githurai All Stars, watacheza na Bentoz United ugenini katika kaunti ndogo ya Roysambu.
  • Victors Faith, mpinzani wao katika fainali za Nairobi Mashariki, atacheza na Ruai FC katika mechi ya kaunti ndogo ya Kasarani.



Wachezaji wakikabiliana Katika Makala ya kwanza ya Sakaja Super Cup
Makala ya pili ya mashindano ya Sakaja Super Cup yamefikia hatua ya mtoano katika kaunti ndogo, huku timu 231 zikichuana kuwania taji hilo.

Mechi zimepangwa kuchezwa Jumamosi na Jumapili wiki hii huku jila kaunti ndogo ikitarajiwa kuwa na timu zisizozidi nane.

Katika kaunti ndogo ya Starehe, Kawasaki na Spade Works FC tayari zimefuzu kwa awamu inayofuata baada ya kukosa wapinzani.

Ajax FC itapimana ubabe na shule ya upili ya Highway, NYS itakaribisha Pelico Jam, huku Autotech ikicheza na Memon FC. MCC itacheza na Sonth B All Stars, Macmilan itaikaribisha City Market, huku TUK Hammers ya Chuo Kikuu cha Ufundi ikimenyana na Riverbank FC.

Katika kaunti ndogo ya Langata, Mtaani FC watawakaribisha Undugu ilhali South C Rangers ikitoa udhia dhidi ya RUSA FC. Wilson Aviators, Wilson FC, na Kings FC zote zinasonga kiotomatiki hadi raundi inayofuata ya mchezo bila kushindana.

Kuwinda United watakuwa wenyeji wa Kuwinda FC. Bomas of Kenya itamenyana na CUK Kysa, huku State City ikitoana kijasho chembamba na Shamah.

Huruma Youth itapania kusonga mbele katika kaunti ndogo ya Nairobi Mashariki watakapomenyana na Sagan City.

Asec Huruma itasafiri hadi Shofco Mathare, huku Mlango Kubwa ikichuana na New Mathare Youngsters.

Kibagare Slums, waliofuzu nusu fainali mwaka jana, watamenyana na Uthiru Vision, huku Kabete Polytechnic wakicheza na Gully Side. Kitisuru All Stars watapimana nguvu na Gachie soccer huku Kipande FC wakiwakaribisha RYSA.

Huko Westlands, timu 16 zitakuwa zikiwinda tiketi ya kusonga mbele kwa raundi inayofuata. Timu Zora nane za Dagoretti Kaskazini tayari zimefuzu kwa ray did ijayo, huku timu 17 kutoka kaunti ndogo zikichuana Dagoretti Kusini.

Katika kaunti ndogo ya Makadara, Mbotela Kamaliza itachuana na Jericho All Stars katika pambano ambalo linaahidi kuwa la kusisimua. Maringo Select itawakaribisha Young Warriors FC, huku Gava FC ikicheza na Makadara Youth.

Vijana wa Komarock watasafiri hadi kaunti ndogo ya Embakasi ya Kati kucheza na Komarock Rangers, ilhali vijana wa Kayole watacheza na Kayole Masters.

Mabingwa watetezi, Githurai All Stars, watacheza na Bentoz United ugenini katika kaunti ndogo ya Roysambu.

Victors Faith, mpinzani wao katika fainali za Nairobi Mashariki, atacheza na Ruai FC katika mechi ya kaunti ndogo ya Kasarani.

Mashindano hayo yanalenga kukuza vipaji mashinani na kuwapa wachezaji wachanga fursa isiyo na kifani ya kuonyesha umahiri wao. Mashindano ya mwaka huu yataanza katika ngazi ya kaunti ndogo na kutumia mfumo wa mtoano.

Michuano hiyo imeandaliwa chini ya ufadhili wa Johnson Sakaja Foundation kwa ushirikiano na Shirikisho la Soka la Kenya matawi ya Nairobi Mashariki na Nairobi West na Serikali ya Kaunti ya Nairobi.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved