logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Trucha akosoa wachezaji wa AFC Leopards

Trucha pia alisema anajivunia pakubwa kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo.

image
na Tony Mballa

Football20 November 2024 - 23:33

Muhtasari


  • Miamba hao wa jadi wa Kenya walianza kampeni yao kwa kasi kwa kuwalaza Mathare United 4-0 katika uwanja wa Dandora.
  • Hata hivyo, baadaye waliandikisha matokeo mseto ambayo yamewaacha katika nafasi ya nne kwenye jedwali baada ya kukusanya pointi 11.

Tomas Trucha




Kocha mkuu wa AFC Leopards, Tomas Trucha, amewataka wachezaji wake kuepuka makosa ya kipuuzi wakati wa mechi za Ligi Kuu ya Kenya.

Miamba hao wa jadi wa Kenya walianza kampeni yao kwa kasi kwa kuwalaza Mathare United 4-0 katika uwanja wa Dandora.

Hata hivyo, baadaye waliandikisha matokeo mseto ambayo yamewaacha katika nafasi ya nne kwenye jedwali baada ya kukusanya pointi 11.

"Lengo letu ni kuepusha makosa yasiyo ya lazima, tumekuwa tukiachana na mabao mepesi katika michezo iliyopita.

Tunatakiwa kuimarika kama timu kwa sababu tumekuwa tukitengeneza nafasi nyingi lakini si nyingi," Trucha alisema.

"Tunahitaji kuchukua nafasi zetu na kuwa macho mbele ya lango ikiwa tunataka kushinda mara kwa mara," aliongeza.

Trucha pia alisema anajivunia pakubwa kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo.

“Kufundisha klabu hizi kunabeba jukumu kubwa, nafurahia hisia hizo kwa sababu zinanipa changamoto, nafurahia kuwa uwanjani na kushiriki michezo hii, nashukuru kuwa katika nafasi hii ambayo makocha wengi wangetamani.

"Kuwa mwanachama wa klabu hii ni heshima kubwa na bahati nzuri. Nataka wachezaji wangu wafanikiwe."

Mkufunzi huyo, raia wa Jamhuri ya Czech, aliwapongeza wafuasi waaminifu wa Ingwe kwa kusimama na klabu hiyo kwa msimu mzima.

"Tuna mashabiki wazuri na michezo iliyohudhuriwa zaidi katika taifa, kama inavyothibitishwa na takwimu za mahudhurio ya uwanja," Trucha alisema.

"Wafuasi wetu wamesimama nasi kwa miaka yote na kuhudhuria michezo yetu kwa wingi, tujaze uwanja, hivyo tafadhali njoo. Tena kwa wingi mnafanya kazi nzuri kama wafuasi wetu, na sasa ni zamu yetu lengo la kupata pointi zaidi katika michezo yetu."


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved