Mchezaji wa Chelsea raia wa Ecuador Moises Caicedo ameelezea furaha yake baada ya mke wake kujifungua mtoto msichana mnamo tarehe 19, Novemba mwaka huu.
Kupitia ukurasa wake wa X, mchezaji huo kiungo cha kati wa Chelsea amechapicha picha na video akiwa na mwanawe mchanga.
Kwenye ujumbe wake, Caicedo amesema kwamba anamshukuru Mungu kwa siku hiyo ya kipekee katika maisha yake akiashiria kuwa mwana aliyezaliwa ndio motisha yake kubwa.
“19/11/2024. Jiunge name kusherehekea na kumshukuru Mungu kwa siku ya kipekee Zaidi katika maisha yangu. Karibu binti mfalme.motisha yangu kubwa.” Aliandika Caicedo kwenye ukurasa wake wa X.
Vile vile, Caicedo mwenye umri wa miaka 23 amemshukuru mpenzi wake Paolita Salazar kwa kumzalia mwana.
“Asante sana mshirika wangu kwa zawadi hii kamili.” Aliongeza kusema Caicedo.
Jumbe za hongera zimeninika kwa mchezaji huyo kwenye mtandao wa Instagram kuanzia Jumatano habari za mkewe kujifungua kuenea mtandaoni.
Mchezaji mwenza katika klabuya Chelsea Pedro Neto amemhongera kwa kusema, “Daddy Moi Congrats.”
Caicedo amesema kuwa mtoto aliyezaliwa ni ongezeko kwa dunia
ya samawati akiashiria klabu ya Chelsea.