logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kevin De Bruyne asimulia kurejea kwake baada ya kukaa nje kwa muda mrefu

Kwa upande wake kocha Pep Guardiola, Kevin De Bruyne anashiriki mazoezi na anayafanya Zaidi ya alivyokuwa akifanya awali.

image
na Brandon Asiema

Football25 November 2024 - 16:39

Muhtasari


  • Kulingana na simulizi yake, Kevin De Bruyne amesema kuwa kuna mengi ya kusimilia ila wakati wa mchuano huo na Brentford, alikosa nguvu za kupiga mpira.
  • Mchezaji huyo amekiri kuwa  kuwa anaweza kuisaidia timu yake kupata matokeo mazuri.


Kiungo wa timu ya Man City Kevin De Bruyne amesema kuwa alihisi vizuri aliporejea kutoka mkekani alikokuwa akiuguza jeraha. Mchezaji huyo amesema kuwa mechi za kwanza tano alizocheza baada ya kupona jeraha zilimfanya kuhisi vizuri sana ila hisia zilibadilika kuwa mbaya timu yake uilipocheza dhidi ya Brentford.

Kulingana na simulizi yake, mchezaji huyo amesema kuwa kuna mengi ya kusimilia ila wakati wa mchuano huo, alikosa nguvu za kupiga mpira. De Bruyne amesema kuwa alikuwa na uwezo wa kufanya mambo mengi kuisaidia timu yake lakini kwenye mchezo huo alikosa uhuru wa  kutamba na kufanya alichokuwa anataka.

Aidha De Bruyne anasema kuwa mapumziko ya kimataifa iliyokuwepo ilimsaidia sana kurejea kwenye hali yake ya kawaidabaada ya kutembelea watu kadhaa waliomsaidia kuhisi vyema.

“Wakati wa mapumziko ya kimataifa, nilitembea kuwaona watu fulani na sasa nimeanza kuhisi vizuri. Umekuwa wakati wa kufadhaisha lakini sasa nahisi bora.” Alisema Kevin De Bruyne.

Hata hivyo, Kevin De Bruyne amesema kuwa anaweza kuisaidia timu yake kupata matokeo mazuri. Kiungo huyo amesema kuwa  anafadhaika kwa sababu ikiwa angalikuwa anahisi vizuri angalikuwa anaisaidia Manchester City lakini kwa hakuwa na uwezo huo.

Kwa upande wake kocha Pep Guardiola, Kevin De Bruyne anashiriki mazoezi na anayafanya Zaidi ya alivyokuwa akifanya awali.



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved