Muungano wa mashirikisho ya soka ukanda wa Afrika Mashariki na kati CECAFA imeweka wazi droo ya kufuzu AFCON ya wavulana wasizoidi umri wa miaka 17 kwa mataiafa wanachama wazi.
Droo hiyo ambayo imefanywa Alhamisi mchana nchini Uganda katika studio za shirikisho la soka nchini Uganda FUFA, imejumuisha jumla ya timu 8 ambazo zimegawanywa kwa makundi mawili yenye timu nne kwa kila kundi.
Kenya imejumuishwa kwenye kundi B pamoja na mabingwa matetezi wa mashindano hayo ya kufuzu AFCON Somalia pamoja na Sudan Kusini na Sudan.
Kwenye kundi A, mataifa ya Uganda, Ethiopia, Tanzania na Burundi yatamenyana ili kupoata mshindi atayefika kwenye fainali.
Wawakilishi watakaowakilisha ukanda wa CECAFA zitakuwa timu mbili ambazo zitacheza fainali ya mechi hizo za kufuzu AFCON.
Michuano
hiyo itaandaliwa nchini Uganda mwezi Disemba kuanzia tarehe 14 hadi 29.