logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Chelsea yamaliza mwezi Novemba bila kupoteza mechi

Katika mashindano yote iliyoshiriki Chelsea, lipata ushindi au sare na wala si kupigwa

image
na Brandon Asiema

Football01 December 2024 - 11:06

Muhtasari


  • Tangu kujiunga na Chelsea mwezi Juni, Maresca ameshinda mechi 6 kati ya 12 na kutoka sare 4 katika ligi kuu nchini Uingereza.
  • Maresca alishinda tuzo ya kocha bora wa mwezi mwezi wa Septemba.


Viwango vya mchezo vya timu ya Chelsea vimeimarika tangu Enzo Maresca kuchukua mikoba ya kuifunza klabu hiyo ya jiji la London mnamo Juni 3, 2024. Maresca alipata fursa ya kuifunza Chelsea baada ya kutimuliwa kwa kocha Mauricio Pochettino kutokana na matokeo mabaya.

Tangu kuingia kwa Maresca, kocha huyo raia wa Italia ameongoza wachezaji wake kwa mechi 12 za ligi kuu nchini Uingereza ambapo katika mechi hizo ameshinda jumla ya mechi 6, kutoka sare mechi 4 na kupoteza mechi mbili pekee.

Katika mwezi wa Novemba, Chelsea haijapoteza mechi hata moja kwenye mashindano yote ambayo Chelsea imeshiriki barani Ulaya. Chelsea imecheza mechi za ligi kuu nchini Uingereza pamoja na mechi ya mashirikisho barani Ulaya maarufu kama Uefa Conference League.

Kwenye mechi ya kwanza ya mwezi Desemba, Chelsea ilitoka sare ya kufungana bao moja dhidi ya Man United, wakati huo kocha Ruben Amorim akiongoza Manchester United kwa mechi yaake ya kwanza ndani ya EPL. Kisha, The Blues waliinyorosha timu ya Noah katika mchuano wa mashirikisho ya Ulaya mabao 8 kwa nunge. Baada ya hapo, sare nyingine ilirekodiwa ugani Stamford Brigde dhidi ya Arsenal ya bao moja, mechi hiyo ikifuatiwa na ushindi mara mbili ugenini wakati Chelsea ilizishinda timu za Leicester na Heidenheim kwa mabao 2 kwa 1 na 2 kwa 0 mtawalia.

Kutokana na matokeo haya mazuri ya Chelsea, kocha Enzo Maresca huenda akatuzwa tuzo ya kocha bora wa mwezi Novemba, tuzo ambayo alishinda katika mwezi wa Septemba.

Mnao Jumapili mwendo wa saa kuni na nusu, Chelsea itamenyana na Aston Villa nyumbani raundi ya 13 ya ligi ya EPL msimu wa 2024/2025.



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved