Jumla ya vilabu 32 kutoka kote duniani vitashiriki kwenye ligi ya dunia kwa vilabu yaani FIFA Club World Cup mwaka.kwa toleo la kwanza litakalofanyika nchini Marekani.
Mashindano haya mapya na yaliyoboreshwa yatapamba jukwaa la dunia mwezi Juni na Julai mwakani, wakati timu 32 zinazoongoza kwenye mashindani ya mabingwa katika mabara yote ya ulimwengu ikiwemo Ulaya, Afrika, Asia, Antartica, Australia, Marekani Kaskazini na Kusini.
Mashirikisho sita ya kimataifa ya soka zimetoa timu mbali mbali kushiriki tukio hilo la kimataifa ambalo litaleta pamoja vilabu vilivyofanikiwa zaidi kutoka kila moja ya mashirikisho ambayo ni : AFC, CAF, Concacaf, CONMEBOL, OFC na UEFA.
Barani Afrika, timu za Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Esperence Sportive de Tunis ya Tunisia na Wydad AC kutoka Casablanca, Morocco zitawakilisha.
Droo ya kombe hilo itaandaliwa jijini Miami nchini Marekani ambapo timu zitakazoshirikizitatambua wapinzani wao kwenye hatua ya makundi mnamo Alhamisi ya Disemba tarehe 5 mwaka 2024.
Timu nyingine maarufu duniani zitaklazoshiriki ni ikiwemo
Chelsea,Man City, Atletico Madrid, Bayern Munich, PSG, Inter Milan, Real Madrid
na Juventus.