Edoardo Bove ambaye ni mchezaji wa ACF Fiorentina ya Serie A nchini Italia anaendelea kupokea matibabu hospitalini kwenye kitengo cha wagonjwa mahututi baada ya kuanguka na kuzirai wakati wa mchuano wa ligi ya Serie kati ya ACF Fiorentina na Inter Milan mnamo Jumapili, Mechi ilikuwa inachezewa katika uga wa nyumbani wa Fiorentina wa Stadio Artemio Franchi.
Kwa mujibu wa ujumbe kutoka klabu ya Fiorentina uliotolewa Jumapili usiku, imesema kwamba hospitali ya chuo kikuu cha Careggi mchezaji huyo anaendelea kupokea matibabu chini ya uangalizi wa karibu wa madaktari kwenye chumba cha wagonjwa mahututi,
Bove alianguka na kuzirai uwanjani jambo ambalo lilipelekea kusitishwa kwa mechi kati ya Fiorentina na Inter Milan. Mchezaji huyo alitibiwa uwanjani kufuatia na kupoteza fahamu kabla ya kupelekwa hospitalini Careggi kwa matibabu Zaidi.
Uchunguzu wa daktari kuhusu hali ya afya ya Bove baada ya kufikishwa hospitalini ulibaini kuwa mchezaji huyo alifika katika idara ya dharura katika hali thabiti ya haemodynamic na vipimo vya awali vya moyo na neva vimeashiria uharibifu mkubwa kwa mfumo mkuu wa neva na mfumo wa kupumua kwa moyo.
Rais wa Fiorentina Rocco Commisso amewashukuru mashabiki na vilabu pamoja na jamii ya soka duniani kwa msaada ulioonyeshwa kwa Edoardo Bove pamoja na familia yake.
Bove alijiunga na Fiorentina mnamo Agosti tarehe 30 kwa mkopo akitokea Roma na kuchezea klabu hiyo mechi ya kwanza mnamo Septemba 15 katika mechi waliopoteza kwa kufungwa mabao 3 kwa 2 dhidi ya Atalanta. Kufikia sasa, mchezaji huyo ameshiriki jumla ya mechi 12 kwa faida ya Fiorentina akifunga bao moja.
Hata hivyo mechi hiyo ilisimamishwa katika dakika ya 16 ya
mchezo baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 kukimbizwa hospitalini.