Mchezaji wa Tusker FC Ryan Wesley Ogam amesema kwamba mabao matatu aliyofunga siku ya Jumapili kwenye mechi ya ligi kuu nchini Kenya kwa faida ya timu yake ya Tusker dhidi Murang’a Seal ni zawadi kwa wazazi wake na mpenzi wake.
Ryan Ogam alifunga mabao hayo matatu maarufu kama hat trick kwenye taaluma ya soka ulimwenguni, magoli ambayo yaliisaidia klabu hiyo ya wanamvinyo kukwea hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo wa jedwali la ligi ya FKFPL.
Akizungumza baada ya mchuano huyo ugani Sportpesa Arena, Ryan aliwashukuru mashabiki waliojitokeza kushabikia timu yao ya Tusker akisema kuwa anahisi vizuri baada ya mchuano huo wa jana. Vile vile alisema kuwa hat trick aliyoifunga inwaendea wazazi wake na mpenzi wake.
“Nahisi vizuri baada ya mchuano wa leo, nashukuru mashabiki kwa sapoti mmetupea leo hapa Murang’a na hii hat trick na-‘dedicate’ kwa wazazi wangu na mtu wangu. Nawapenda sana.” Alisema Ryan Wesley Ogam.
Hat trick hiyo ya
Ogam ni ya kwanza katika taaluma yake tangu kujiunga na timu ya ligi kuu nchini
FKFPL.
Kufikia sasa, Tusker inashikilia nafasi ya tatu kwa alama 18 baada ya mechi 10 za ligi msimu huu wakiwa na mechi moja mkononi.