Seneta wa kaunti ya Nandi Samsom Cherargei amekashifu utendakakazi wa gavana wa kaunti hiyo Stephen Sang akimlaumu kudhoofisha maendeleo na ukuaji wa kaunti hiyo.
Kwa mujibu wa seneta Sang, amesema kuwa mara nyingi amekuwa akishinikiza kuwa ndani ya uongozi wa gavana huyo, huduma za afya katika hospitali ya rufaa ya Kapsabet na vituo vingine vya afya katika kaunti ya Nandi zimedorora. Sang amesema kwamba hospitali hiyo ya rufaa ya kaunti ya Nandi imegeuka na kuwa sehemu ya uhalifu.
Seneta huyo amesema kwamba hospitali ya Kapsabet imekosa vifaa muhimu vya matibabu ikiwemo glavu na sindano huku wagonjwa wakitumwa kununua dawa katika katika maduka ya dawa ya watu binafsi.
Kwenye ukurasa wake wa X, seneta Cherargei alisema kwamba alifanya ziara ya kushtukiza katika hospitali hiyo mnamo Jumapili jioni na kueleza kwamba hali aliyokumbana nayo ilikuwa ya kiwewe akipigia mfano namna miradi ya maendeleo katika sehemu mbali mbali za kaunti hiyo zimekosa kufanyika.
Cherargei amemsuta Sang akisema kuwa wiki iliyopita, alizindua dawa za uzazi ikiwemo kondomu na dawa za kupanga uzazi zenye thamani ya shilingi milioni 48 badala ya kushughulikia vifaa vingine vya afya vya msingi.
Katika ripoti ya seneta Cherargei baada ya kutembelea hospitali hiyo, alisema kuwa kunakosekana matabibu wa kutosha, hali mbaya ya usafi, wadi zilizojaa wagonjwa kwenye vitanda vibovu pamoja na ukosefu wa mwangaza wakati wa usiku.
Hata hivyo seneta huyo amependekeza kubanduliwa kwa gavana Sang, kutokana na maendeleo duni, utawala mbovu na ukiukaji wa haki za kibinadamu.
Vile vile ameomba
kamati ya afya kwenye bunge la seneti kuzuru hospitali ya rufaa ya Kapsabet ili
kutoa mwelekeo unaostahili.