Msimamo wa jedwali la ligi za Uingereza na Uhispania zinazidi kubadilika kila baada ya angalau siku nne kutokana na michuano zinazochezwa katikati ya wiki, ushindani mkali ukizidi kuonekana hasa katika nafasi ya kufuzu kombe la klabu bingwa barani Ulaya.
Katika ligi ya Uingereza timu ya Liverpool inasalia kileleta kwa jedwali kabla ya mchuano wake dhidi ya Newscastle kwa alama 34. Liverpool imesalia uongozini mwa jedwali licha ya kutoka sare ya kufungana mabao 3 kwa 3 katika mechi ya Jumatano usiku iliyochezwa ugani St James Park.
Katika mechi sita za Liverpool za awali, mabingwa hao wa EPL msimu wa 2019/2020 imeshinda mechi tano na kutoka sare mechi moja. Timu hiyo chini ya kocha Arne Slot sasa imeweka mwanya wa alama 7 kati yake na Chelsea wanaoshikilia nafasi ya 2.
Timu ya Chelsea ilipata ushindi muhimu wa mabao 5-1 dhidi ya Southamptom ugenini St Marys. Ushindi huo uliwaweka katika nafasi juu ya Arsenal ambayo inashikilia nafasi ya 3 kwa uchache wa mabao licha ya kutoshana na Chelsea kwa takribani kila kitengo. Kwenye mechi hiyo, mchezaji J. Stephens wa Southampton alipokezwa kadi nyekundu katika dakika ya 39 mchezo huo.
Kwenye matokeo mengine, mechi kati ya Arsenal na Manchester United iliishia kwa ushindi wa faida ya timu ya Arsenal. Ushindi huo wa mabao mawili kwa nunge kuliiweka Arsenal katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa jedwali kwa alama 28.
Manchester United baada ya kichapo hicho ilishuka nafasi mbili jedwalini na kutua katika nafasi ya 11 kwa alama 19.
Kwenye kambi ya Etihad, hatimaye jeshi la Manchester City linaloongozwa na kocha Pep Guardiola lilipata ushindi wake wa kwanza ndani ya mechi 5 za awali. Ushindi huo wa mabao 4 kwa matatu kwa sufuri dhisi ya Nottingham Forest umewaweka katika nafasi ya 4 jedwalini.
Nchini Uhispania, ligi ya La Liga inazidi kupamba moto Barcelona, Real Madrid na Atletico Madrid zikibanana katika nafasi za tatu za kwanza. Barcelona inaongoza jedwali la La Liga kwa alama 37. Barcelona sasa liko juu ya Real Madrid ambayo ipo katika nafasi ya pili kwa alama 33, hii ni baada ya Madrid kupoteza mchuano yao dhidi ya Athletico Bilbao kwa 2-1.
Timu ya Atletico Madrid inashikilia nafasi ya tatu na alama 32 wakiratibiwa kuvaana na Sevilla mnamo Jumapili 8, Disemba 2024 ugani Wanda Metripolitano
Timu ya Athletic Bilbao inashikilia nafasi ya nne baada ya kuicharaza Real Madrid mabao 2-1, Bilbao wameandikisha ushindi tano na sare moja katika mechi zao sita za awali.
Kwenye ligi za La Liga na EPL, timu zilizo katika mabano ya nne bora zinaachana kwa alama kidogo.