Klabu ya Chelsea imeendeleza msururu wa matokeo bora kwenye ligi kuu ya Uingereza baada ya kutoka nyuma na kuicharaza Tottenham Hotspur mabao manne kwa matatu katika mechi ya raundi ya 15 ya msimu 2024/2025.
Chelsea chini ya kocha Enzo Maresca imedumisha viwango vyake vya mchezo huku ikipanda jedwali hadi nafasi ya pili kwa alama 31 mbele ya Arsenal iliyotoka sare ya kufungana mabao 1 kwa 1 dhidi ya Fulham. Liverpool inazidi kushikilia nafasi ya kwanza kwa alama 35 licha ya kucheza mechi chache kuliko Chelsea na Arsenal.
Timu za Chelsea kwa upande wa wanaume na wanawake, tangi msimu wa 2024/2025 kung’oa nanga, zimekuwa zikirekodi matokeo bora kwenye ligo zote ambazo zinashiriki.
Katika mechi ya wikendi iliyopita, Chelsea ya wanawake iliicharaza Brighton & Hove Albion mabao 4 kwa 2 katika ligi kuu ya wanawake nchini Uingereza.
Kufikia sasa, Chelsea ya wanawake inaongoza ligi hiyo kwa alama 27, alama 5 juu ya nafasi ya pili Manchester City. Timu hiyo imecheza jumla ya mechi 9 ikiwa imeshinda mechi tano za awali huku Man City ya wanwake ikiwa imepoteza mechi moja kati ya tano za awali.
Kwa upande wa wanaume, Chelsea imetoka sare mechi 1 na kushinda nne kati ya mechi tano za awali.
Timu hizi mbili, zilishinda mechi ya wikendi iliyopita kwa mabao manne kila mmoja.
Msimu huu, kufikia sasa, timu ya Chelsea ya wanawake
imekusanya jumla ya magoli 41 katika mashindano yote huku Chelsea ya wanaume
ikikusanya magoli 61 kwenye mashindano yote. Kwenye ligi kuu ya wanawake
Uingereza, Chelsea ya wanawake ina alama 27 ikiongozwa jedwali hilo baada ya
mechi 9 huku wenzao wa kiume wakiwa na alama 31 baada ya raundi 15 za msimu 2024/2025.