Klabu ya Uingereza ya Liverpool, imezidi kuandikisha matokeo bora katika mashindano ya klabu bingwa barani Ulaya kufikia sasa ikiwa haijapoteza wala kutoka sare katika michuano 6 kati ya 8 ambazo imecheza.
Liverpool inaongoza msimamo wa jedwali hilo kwa jumla ya alama 18 ikiwa ni nafasi ya moj akwa moja ya kufuzu awamu ya kumi na sita bora.
Miamba hao wa soka nchini Uingereza wanaonyesha nia ya hamu ya kutwaa taji hilo kubwa baada ya kulipoteza kwenye fainali ya klabu bingwa barani Ulaya katika msimu wa 2021/2022 kwa Real Madrid.
Klabu hiyo katika historia yake kwenye kipute cha Klabu bingwa barani Ulaya, wametwaa taji hilo mara sita. Liverpool ilinyakua kombe hilo mara ya kwanza msimu wa 1976/77 na kulitwa tena mara ya pili mfululizo katika msimu uliofuata wa 1977/1978.
Mbali na kuweka matokeo mazuri kwenye kipute hicho, Liverpool pia inaandikisha matokeo ya kufurahisha mashabiki wake kwenye ligi kuu ya Uingereza ikiwa inashikilia nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa jedwali.
Kwenye EPL, baada ya mechi 14 za msimu huu, klabu hiyo inaongoza kwa alama 35 ikiwa na mchuano mmoja mkononi ambao ulihairishwa kutokana na hali mbaya ya hali ya hewa iliyoshuhudiwa katika baadhi ya sehemu nchini Uingereza mnamo Jumamosi.
Liverpool imepoteza mechi moja pekee yake, kutoka sare mechi
mbili na kushinda mechi kumi na moja kwenye ligi kuu ya Uingereza msimu huu
2024/2025.