Baada ya vilabu vikubwa katika ligi kuu nchini Uingereza kufukuzia saini ya mchezaji Emmanuel Ziro mzawa wa Kenya kutoka kaunti ya Kilifi, hatimaye klabu ya Manchester United imefanikiwa kumpata kinda huyo mwenye numri wa miaka 16. Ziro amekuwa akitafutwa na vilabu vya Arsenal na Chelsea kutoka academia ambayo amekuwa akinoa talanta yake.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Ziro ameishukuru familia yake kwa mapenzi na sapoti pamoja na motisha waliyompa katika miaka yake kwenye academia ya soka ya cre8tive.football.
Ziro amefurahia fursa aliyoipata kuchezea Manchester United, klabu aliyosema kwamba amekuwa akitamani sana kuichezea.
“Sasa nina nafasi ya kuendelea kucheza soka katika klabu kubwa duniani. timu ambayo pia nashabikia.” Alisema Emmanuel Ziro.
Aidha kwa mujibu wa risingballers, pia ilichapisha picha
kwenye ukurasa wake wa Instagram ikisema kwamba Mchezaji huyo kiungo cha kati aliamua
kutia sahihi na klabu ya Manchester United baada ya baadhi ya klabu kubwa nchini
Uingereza kumtaka.
“Emmanuel Ziro ameamua kutia sahihi na
Manchester United baada ya vilabu kubwa Uingereza kuonyesha nia ya kumchukua.
Ametoka chini hadi kwa mojawapo wa academia nzuri duniani. Inaonyesha chochote
kinawezekana.” Iliandika Rising Ballers kwenye ukurasa wake
wa Instagram.