Mashabiki wa kabumbu katika ligi kuu nchini Kenya wametoa mseto wa hisia kuhusu mchuano kati ya Gor Mahia na Shabana ambayo imeratibiwa kuchezwa Jumatano kuanzioa saa kumi jioni katika uwanja wa Kenyatta mjini Machakos.
Baada ya kampuni ya kupeperusha matangazo na picha za moja kwa moja za ligi kuu nchi FKFPL kuchapisha picha ya kuuza mchuano huo, mashabiki wa soka walijibu kwenye chapisho hilo kauli mbali mbali kuhusu mchexo huo.
Katika bango lililochapishwa na Azam Sports Ke, mchuano huo ulitajwa kuwa debi ya mkoa wa Nyanza.
Mtumiaji mmoja wa mtandao wa X, alishangazwa na jinsi mchunao mkubwa kama huo unaweza kuratibiwa kuchezwa siku ambayo ni kati kati ya wiki kwa maana ya Jumatano.
“Mbona tuwe na mchuano mkubwa hivo kati kati ya wiki jamani? Aliuliza Lameck Mogere. Hata hivyo Azam Sports Ke ilimjibu ikisema kwamba ni ratiba tu!
Kwenye chapisho hilo, mashabiki walionekana kushangazwa na mechi hiyo kuitwa ‘Nyanza Derby’ maoni mbali mbali yakitolewa kuhusiana na mechi hiyo.
“Nyanza Derby ndio nini?” Aliuliza Van Okush
“Gor Mahia ni timu ya Nairobi, nyanza nini.” Alisema jah messenger.
“What’s Nyanza Derby?” Aliuliza Izc Ivan.
Aidha katika ratiba ya michuano mingine ya Jumatano ni kwamba
- FC Talanta VS Mara Sugar (Machakos) 1pm
- Kariobangi Sharks VS Nairobi City Stars – Dandora) 1pm
- Bidco United VS Police FC (Sportpesa Arena) 1pm
- Ulinzi Stars VS Bandari FC (Kinoru) 4PM
- Posta Rangers VS Kakamega Homebpoyz (Sportpesa Arena) 4pm
- Afc Leopards VS Tusker (Dandora) 4pm
- Gor Mahia VS Shabana (Machakos) 4pm
Mnamo Alhamisi Disemba 12, mechi moja itachezwa
ambapo KCB itawakaribisha Sofapaka katika uga wa Sportpesa Arena mwendo wa saa
tisa adhuhuri