Katika michuano zilizoandaliwa hapo tarehe 10,12.2024. Timu ya Liverpool iliendelea kuandikisha matokeo bora hii ni baada ya kuicharaza Girona bao moja kavu ugani Municipal de Montilivi bao lililopachikwa na Salah kupitia mkwaju wa penalti katika dakika ya 63. Liverpool bado linaongoza katika jedwali wakiwa na pointi 18 huku Girona ikishikilia nafasi ya 30 na pointi 3 baada ya kucheza mechi sita.
Timu ya uingereza iliyoandikisha ushindi ni pamoja na Aston Villa baada ya kuilaza RB Leipzig mabao matatu kwa mbili 3-2 ugani Leipzig Stadium. Ushindi huo unaiweka Aston Villa katika nafasi ya 3 kwenye jedwali wakiwa na alama 13. Villa walipoteza mechi yao dhidi ya Club Brugge na kutoka sare dhidi ya Juventus. RP Leipzig wanashikilia nafasi ya 34 baada ya kucheza mechi 6 na kukosa kuandikisha alama katika mechi hizo sita.
Mabingwa wa mashindano hayo wa mwaka wa 2024, Real Madrid walipata ushindi dhidi ya Atalanta wa mabao tatu kwa mbili 3-2, ugani Gewiss. Bao la ufunguzi lilifungwa na nyota K. Mbappe katika dakika ya 10, Vinicious akifuata na bao la pili katika dakika ya 56 huku J. Bellingham akifunga bao la mwisho katika dakika ya 59. Madrid inashikilia nafasi ya 18 na pointi 9, pointi 9 nyuma ya Liverpool wanaoshikilia nafasi ya kwanza, na pointi 3 nyuma ya maasidi wao Barcelona ambao wanashikilia nafasi ya sita na pointi 12.
Timu ya Bayern Munchen ambayo imeandikisha ushindi katika mchuano zake tatu za awali walipata nafasi ya kuiadhibu Shakhtar Donetsk mabao tano kwa moja 5-1. Ugani veltis Arena . K. Laimer alipata bao la ufunguzi dakika ya 11 akifuata T. Muller mnamo dakika ya 45 na bao la pili huku M. Olise akifunga bao la tatu katika dakika ya 70 kupitia matuta ya penalti na la tano katika dakika ya 90+3. J. Omusialla alipachika bao la nne katika dakika ya 84. Munchen wanashikilia nafasi ya 8 huku wakiwa na pointi 12. Shakhtar wanashikilia nafasi ya 27 na pointi 4 kwenye jedwali.
Timu ya Pari Saint Germain waliipiga Red Bull Salsburg mabao 3-0, P.S.G. wanashikilia nafasi ya 24 na pointi 7 huku Salsburg wakishikilia nafasi ya 32 na pointi 3. Kwingineko ni kuwa timu ya Bayer Leverkusen ilipata ushindi ya bao 1-0 dhidi ya Inter Milan, Leverkusen wanashikilia nafasi ya pili kwenye jedwali wakiwa na pointi 13 ikiwa ni pointi 5 nyuma ya Liverpool wanaongoza jedwali hilo huku Millan wakiwa katika nafasi ya 4 na pointi 13.
Timu ya Leipzig sasa italazimika kujiondoa katika mashindano hayo baada ya kushindwa kuandikisha ushindi hata mmoja huku Liverpool wamejikatia tikiti ya kushiriki katika awamu ya 16 ama awamu ya mchujo.
Katika mabadiliko yaliyofanyika timu nane bora watafuzu moja kwa moja katika raondi ya 16, huku wenye watamaliza katika nafasi ya 9 hadi 24 watapigania raondi ya mchujo huku mwenye atashinda atafuzu kuingia katika raondi ya 16.