Klabu ya Wolves inayoshiriki Ligi Kuu ya Uingereza imemfuta kazi kocha mkuu Gary O'Neil kufuatia kipigo kibaya nyumbani dhidi ya Ipswich siku ya Jumamosi.
Ripoti kutoka Ulaya zinaonyesha kuwa kocha huyo mwenye umri wa miaka 41 alitimuliwa Jumapili asubuhi kufuatia mfululizo wa matokeo mabaya ya klabu hiyo.
Kipigo cha mabao 2-1 kwenye Uwanja
wa Molineux Jumamosi jioni, ambacho kilifuatiwa na mvutano ambao ulimfanya
Rayan Ait-Nouri kuondolewa uwanjani, kiliiacha Wolves katika nafasi ya 19
kwenye jedwali la Ligi Kuu.
Kuondoka kwa O'Neil katika Molineux kunakuja baada ya timu yake kupata ushindi mara mbili pekee kati ya mechi 16 za Ligii Kuu zilizochezwa, na kuwaacha Southampton pekee waliopanda daraja hivi majuzi chini yao kwenye msimamo wa Ligi Kuu.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 41 alikosoa sana uchezaji wa timu yake dhidi ya Ipswich, akidai kwamba hakuna kitu ambacho angeweza kufanya kuhusu wachezaji wake kutochukua nafasi zinazofaa kabla ya Jack Taylor kufunga bao la kwanza.
Kumekuwa na matukio mengi katika siku za hivi karibuni ambayo yameonyesha kuchanganyikiwa kwa timu hiyo. Kiungo Mario Lemina alivuliwa kitambaa cha unahodha mapema wiki hii baada ya kugombana na nahodha wa West Ham Jarrod Bowen Jumatatu usiku.
Hali ya hasira iliendelea kupamba moto wikendi, huku Rayan Ait-Nouri akilazimika kutolewa nje ya uwanja na mchezaji mwenzake Craig Dawson, huku mshambuliaji nyota Matheus Cunha akikabiliwa na adhabu ya hapo awali kutoka kwa FA baada ya kugombana kimwili na mchezaji wa Ipswich.
O'Neil aliiongoza Wolves hadi nafasi ya 14 msimu uliopita, lakini alishuhudia wachezaji nyota Pedro Neto na Max Kilman wakiondoka kwenda Chelsea na West Ham msimu wa joto