Rais wa shirikisho la soka nchini FKF Hussein Mohamed amefichua kwamba shirikisho analoongoza litashirikiana na shirikisho la soka duniani FIFA kujenga kituo cha kiufundi nchini katika siku za usoni.
Hussein Mohamed alidhibitisha hilo kupitia ukurasa wake wa X ambapo alichapisha picha akiwa pamoja na rais wa FIFA Gianni Infantino katika sherehe za tuzo za shirikisho la soka barani Afrika CAF za mwaka 2024 zilizofanyika Marrakech nchini Morocco.
Kwa mujibu wa Hussein Mohamed, ujenzi wa kituo hicho baada ya kukamilika utasaidia katika kuimariosha na kukuza mchezo wa kandanda nchini Kenya.
Pia, Mohammed alisema kwamba yeye pamoja na Infantino walijadili masuala muhimu kuhusu kandanda laKenya kwa wanaume na wanawake na jinis ya kuimarisha mchezo huo.
Katika mkutano waliofanya na rais wa FIFA, Hussein Mohammed amesema kwamba majidiliano yao yalikita katika maswalaya uongozi, miundo misingi ya soka na ukuaji wa soka nchini Kenya.
Ziara ya Hussein Mohammed nchini Morocco ndio ilikuwa yake ya kwanza ya rasmi tangu achukue uongozi wa shirikisho nchini katika uchaguzi wa Disemba 7, 2024, baada ya kuwashinda wapinzani wake ikiwemo naibu rais na rais watangulizi wake Doris Petra na Nick Mwendwa.
Hussein Mohammed alikuwa ameandamana na naibu wake MacDonald
Mariga kwenye hafla hiyo ya CAF Awards.