Mshambulizi wa klabu ya Chelsea Mykhailo Mudryk huenda atapata pigo la kuhudumia marufuku ya kutocheza kabumbu kwa miaka kadhaa ikiwa uchunguzi wa pili wa mkojo wake utabaini kwamba alitumia dawa zilizopigwa marufuku.
Ikidhibitisha uchunguzi uliofanywa na shirikisho la soka nchini Uingereza FA, Chelsea imesema kwamba FA, iliwasiliana na Mykhailo Mudryk kuhusu upatikanaji wa chembechembe za dawa zilizopigwa marufuku kupatikana katika mkojo uliofanyiwa uchunguzi.
Hata hivyo, usimamizi wa Chelsea na Mykhailo kupitia ujumbe kwa vyombo vya habari, imesema kwamba inaunga mkono programu ya FA kufanya uchunguzi kwa wachezaji wote kila mara.
Aidha kwa upande wa Mykhailo, amedhibitisha kupokezwa taarifa hiyo ya upatikanaji wa dawa zilizopigwa marufuku akisema kwamba hajawai kwa wakato wowote ule kutumia dawa haramu kwa kujua.
Mykhailo amesema kwamba habari hizo zimemfikia kwa mshtuko akiamini kwamba hajafanya lolote kinyume na sheria.
“Hii limefika kwangu kwa mshtuko kwani sijawahi kwa kujua kutumia dawa
zozote zilizopigwa marufuku wala kuvunja
sheria zozote…” Alisema Mudryk
kwenye ukurasa wake wa Instagram Jumanne mchana.
Mykhailo pamoja na Chelsea hata hivyo wamesema kwamba hawatatoa taarifa nyingine zaidi kuhusu swala hilo.
Kwa mujibu wa mtandao wa Daily Mail kuna imani kwamba upatikanaji wa chembechembe hizo unaweza kuwa umetokea nje ya Uingereza kwa sababu dawa iliyopatikana kwenye sampuli ya Mudryk haipatikani nchini Uingereza.
Mudryk bado anasubiri matokeo ya sampuli ya ‘B’ na iwapo
yatathibitisha au la matokeo ya sampuli yake ya ‘A’ atakuwa anachungulia
marufuku ya hadi miaka minne.