Kipute cha mashirikisho cha UEFA kitazidi kupamba moto usiku wa Alhamisi, Disemba 19 wakati mechi za raundi ya 6 zitachezwa katika viwanja mbali mbali barani Ulaya.
Mechi ambayo itaangaziwa mno na wapenzi wa soka ni baina ya viongozi wa ligi hiyo Chelsea ambao pia wanazidi kuandikisha matokeo ya kuridhisha kwenye ligi kuu nchini Uingereza na timu ya Shamrock Rovers ya Ireland wanaoshikilia nafasi ya 6 kwenye msimamo wa jedwali la kombe la mashirikisho.
Timu hizo mbili kufikia mechi ya raundi ya 5, hazijapoteza mechi yoyote. Chelsea imeshinda michuano yote 5 ilizocheza nyumabni na ugenini huku Shamrock Rovers wakiwa wameshinda mechi tatu na kutoka sare mechi 2.
Kwenye kombe la mashirikisho ya UEFA, ni timu tatu pekee ambazo hazijapigwa kwenye mechi zao ambazo ni Chelsea walioshoinda mechi zote, Vitoria SC ambao wametoka sare mechi moja na Shamrock Rovers ambao wameshinda mechi 2 na sare mechi mbili.
Ligi hiyo iliyoasisiwa mwaka 2021, inajumuisha timu 36 sawia na mpangilio wa ligi ya mabingwa barani Ulaya ambapo timu za kwanza 8 zitafuzu moja kwa moja kwa hatua ya 16 bora huku timu zitakazomaliza katia ya nafasi ya 9 na 24 zitacheza michuano miwili(nyumbani na ugenini) baada ya droo kufanyika.
Mechi hiyo kati ya Chelsea na Shamrock Rovers itachezwa
Alhamisi ugani Stamford Bridge kuanzia saa tano usiku.