Mchezaji nyota wa timu ya taifa ya Nigeria Ademola Lookman alitawazwa Mwanasoka Bora wa Afrika 2024 kwenye Hafla ya Tuzo za Shirikisho la Soka Afrika (Caf) iliyofanyika mjini Marrakesh, nchini Morocco.
Mshambuliaji huyo wa klabu ya Atalanta alikuwa akipambania tuzo hilo na Simon Adingra wa Ivory Coast, Serhou Guirassy wa Guinea, Achraf Hakimi wa Morocco na Ronwen Williams wa Afrika Kusini.
Lookman ni Mnigeria wa pili mfululizo kutwaa tuzo hiyo baada ya Victor Osimhen kushinda mwaka 2023.
Mshambulizi wa timu ya wanawake ya Orlando Pride Barbra Banda aliweka historia ya kuwa Mzambia wa kwanza kushinda tuzo ya wanawake, akimaliza mbele ya Mmorocco Sanaa Mssoudy na Chiamaka Nnadozie wa Nigeria.
Washindi hao hupigiwa kura na jopo la wataalamu ambalo linajumuisha wajumbe wa kamati ya ufundi ya Caf pamoja na wanahabari wa Afrika, wachezaji na makocha.
Tazama orodha ya washindi wengine wa tuzo mbalimbali;
1.
Mchezaji Bora wa Mwaka kwa Wanaume - Ademola Lookman (Atlanta, Nigeria)
2.
Mchezaji Bora wa Mwaka kwa Wanawake - Barbra Banda (Orlando Pride, Zambia)
3.
Kocha Bora wa Mwaka kwa Wanaume - Emerse Faé (Côte d'Ivoire)
4.
Kocha Bora wa Mwaka kwa Wanawake - Lamia Boumehdi (TP Mazembe; Morocco)
5.
Golikipa Bora wa Wanaume wa Mwaka - Ronwen Williams (Afrika Kusini, Mamelodi)
6.
Golikipa Bora wa Mwaka wa Wanawake - Chiamaka Nnadozie (Nigeria)
7.
Mchezaji Bora wa Mwaka wa Klabu kwa Wanaume - Ronwen Williams (Afrika Kusini,
Mamelodi)
8.
Mchezaji Bora wa Mwaka wa Klabu kwa Wanawake - Sanâa Mssoudy (Morocco, AS FAR)
9.
Mchezaji Bora Chipukizi wa Mwaka kwa Wanaume - Lamine Camara (Senegal, Monaco)
10.
Mchezaji Bora Chipukizi wa Mwaka kwa Wanawake - Doha El Madani (Morocco, AS FAR)