Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 aliwania tuzo hiyo na wachezaji wenzake wa timu ya taifa Dejan Kulusevski ambaye aliwahi kupokea tuzo hiyo kwa awamu mbili mfululizo zilizopita na Alexander Isak, pamoja na Isak Hien.
Viktor Gyokeres amepokea tuzo hiyo siku moja baada ya kupokea tuzo ya mshambuliaji bora wa mwaka nchini kwao. Ushindi wa tuzo hiyo ya mshambulizi bora wa mwaka ulikuwa wa pili Gyokeres kuipokea kwani alishinda tuzo hiyo mwaka jana.
Viktor Gyökeres anapokea Mpira wa Dhahabu kwa uchezaji wake bora katika timu ya klabu ya Sporting CP na timu ya taifa akisema kwamba ubora wake umedhihirika sio tu nchini Ureno bali pia katika bara la Ulaya kwa ujumla.
Mchezaji huyo ana mabao 15 Katika mechi 26 za kimataifa ambapo bao zake kumi zimekuwa chini ya mkufunzi mpya wa Uswidi Jon Dahl Tomasson.
Nyota huyo wa Uswidi alisema kuwa anamatumaini ya kuendelea na matokeo bora licha ya kutocheza katika ligi ya premia kama wenzake.
‘’Sichezi Ligi ya Premia kama wengine wanavyofanya, lakini nimefanya vyema kabisa nilipo. Na nadhani nimejidhihirisha katika ligi ya ulaya pia, kwenye Ligi ya Mabingwa. Na timu ya taifa. Hivyo si tu katika Ureno,’’ Alisema Gyokeres.
Mpira wa Dhahabu hutunukiwa mchezaji bora wa kiume katika soka ya Uswidi na umetolewa na Chama cha Soka cha Uswidi tangu 1946.
Zlatan Ibrahimovic ametuzwa tuzo hiyo mara mingi zaidi, jumla ya Mipira kumi na mbili katika kipindi cha 2005-2020.
Hii ndio mara ya kwanza katika maisha yake kama mchezaji Viktor Gyokeres anapata tuzo hili la mpira wa dhahabu.
Gyokeres alizaliwa 4, Juni 1998 jijini Stockholm sasa anaichezea klabu ya sporting Lisbon kama mshambulizi ikiwa hapo awali ameichezea timu ya Brighton, Swansea na Coventry miongoni mwa timu nyingine.
Akiwa na bao la Jumapili dhidi ya Boavista bao lake la 18 kwenye ligi kwa msimu huu - sasa yuko kwenye kikundi kidogo cha wachezaji wa kipekee wa kandanda. Kwa kuwa na bao 61 kuonekana kwa mwaka wa kalenda, inamaanisha kuwa alikua mchezaji wa nane wa muda wote kufikia mafanikio ya kufunga zaidi ya mabao 60.