Katika hatua inayolenga kuimarisha safu ya ushambulizi wake, klabu ya Arsenal inalenga kupata sahihi ya mchezaji wa RB Leipzig Benjamin Sesko katika dirisha la uhamisho linalotarajiwa kufunguliwa mwakani baada ya mshambuiliaji wa Sporting CP Viktor Gyokeres kuonyesha nia ya kusalia klabuni anakocheza sasa.
Kwa mujibu wa jarida la Football Transfers, Mikel Arteta amebadili mawazo yake na kuyaelekeza zaidi kwa Benjamin Sesko ambapo awali klabu hiyo ya London ilimtaka sana Gyokeres. Hata hivyo, Arsenal ingali kwenye mazungumzo na Viktor Gyokeres licha ya kumtaka Benjamin Sesko pia.
Benjamin mwenye umri wa miaka 21, anadaiwa kuwa chaguo la kwanza kwa Arteta kutokana na makali yake msimu huu ambapo katika mechi 23 alizochezea RB Leipzig amefunga magoli 11 kufikia sasa.
Hata hivyo licha ya Viktor Gyokeres kuonekana kutaka kusalia Ureno na Sporting CP, matumaini ya Arsenal kumpata huenda yakakatizwa na klabu ya Manchester United ambapo Football London inaarifu kwamba ikiwa atahamia kwenye ligi ya Primia, Manchester United ndio watapata saini yake.
Awali Arsenal ilitaka kupata huduma za Kolo Muani ila
imebadilisha nia na kuwaangazia Benjamin Sesko na Viktor Gyokeres baada ya Kolo
Muani kuonekana kuegemea sana upande wa AS Monaco.
“Hakuna pendekezo la sasa kwamba watajaribu
kumsajili fowadi huyo mwezi Januari. Mshambulizi huyo wa kati mwenye umri wa
miaka 26 kwa sasa anajikuta kwenye ukingo wa timu ya Luis Enrique na
anatarajiwa kuondoka msimu huu wa baridi.” Mwandishi wa habari za michezo wa The Athletics aliripoti.