logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Tetesi za uhamisho barani Ulaya: Lamine Yamal anakaribia kuongeza mkataba na Barcelona hadi 2030.

Mkataba wa sasa wa Yamal na Barcelona unatarajiwa kukamilika mwaka 2026

image
na Brandon Asiema

Football23 December 2024 - 16:30

Muhtasari


  • PSG nao wamearifiwa kuwa wapo tayari kutoa Yuro milioni 83 kwa ajili ya Alexander Isak wa Newscastle.
  • Lamine Yamal ambaye thamani yake inadaiwa kuwa Yuro milioni 150, tayari ana mkataba na Barcelona unaokamilika mwaka wa 2026.


Winga, kinda wa Barcelona na timu ya taifa la Uhispania Lamine Yamal anakaribia kurefusha mkataba wake na Barcelona hadi mwaka 2030. Hii ni kwa mujibu wa wakala wa soka wa Uhispania Nicolo Schira. Lamine Yamal ambaye thamani yake inadaiwa kuwa Yuro milioni 150, tayari ana mkataba na Barcelona unaokamilika mwaka wa 2026.

Hata hivyo, klabu hiyo inayoshikilia nafasi ya 2 kwenye msimamo wa jedwali ya La Liga msimu huu kufikia Jumatatu Disemba 23, huenda ikamwachilia kiungo wake wa kati Frenkie de Jong raia wa Uholanzi katika uhamisho wa mwakani.

Katika kambi hiyo ya Camp Nou, Eric Garcia anapigania kuwa na nafasi yake kwenye klabu hiyo jarida la Sport – in la Uhispania likiripoti kuwa Newscastle imeonyesha nia ya kumsaini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23. Beki huyo aliwahi kucheza katika ligi ya Primia akihudumia timu ya Manchester United.

Nchini Uingereza, Crystal Palace wanafukuzia saini ya Jan-Niklas Beste mwenye umri wa miaka 25 kutoka ligi ya Ureno anakochezea Benfica. Hii ni kwa mujibu wa Sky Sports Uswisi.

Liverpool nao watalazimika kungojea hadi majira ya joto ili kufanikisha kupata huduma za Joao Pedro raia wa Brasil kutoka Brighton & Hove Albion. Jarida la Football Insider linaarifu kuwa mahitaji ya Brighton kwa mchezaji huyo wa miaka 23 ni magumu kwa Liverpool kuafikia katika dirisha la uhamisho la Januari.

Real Madrid kwa upande wao wanalenga kumrejesha Rafa Marin mwenye umri wa miaka 22 anayechezea Napoli kwa sasa. Rafa aliwahi kuwa katika mazoezi na timu ya vijana ya Real Madrid.

PSG nao wamearifiwa kuwa wapo tayari kutoa Yuro milioni 83 kwa ajili ya Alexander Isak wa Newscastle.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved